09 September 2013

MEMBE AJITETEA JIMBONI



 Na Said Hauni, Lindi
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Benard Membe, amewaomba radhi wananchi wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi kwa kutoonekana jimboni kwake muda mrefu.Alisema hali hiyo imechangiwa na majukumu aliyonayo kitaifa, kimataifa na kuahidi kutumia muda wa likizo kufanya ziara katika jimbo hilo ili aweze kuzungumza na wananchi
.Bw. Membe aliyasema hayo juzi wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi ili kumpata Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) wa chama hicho, uliofanyika kwenye Kata ya Kiwalala, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi.
A l i s e m a m a j u k u m u aliyoongezewa serikalini, yamechangia kwa kiasi kikubwa kutofika jimboni kwake mara kwa mara hivyo hutuia muda mwingi kutekeleza majukumu hayo."Si kwamba nafanya makusudi, leo nimewaomba radhi lakini simaanishi kuanzia sasa muda wote nitakuwa jimboni si kweli, nazungumza hivi ili mnielewe," alisema Bw. Membe.
Alisema yeye ataendelea kuwapenda wapigakura wake ambao ndio waliompa nafasi ya kuwa mbunge wao hivyo kutoonekana kwake jimboni kusiwanyong'onyeze.Wakati sijaongezewa majukumu, nilikuwa nakuja kila mwezi lakini hivi sasa nashindwa kufanya hivyo, nimeelemewa na mzigo mzito, baadhi yenu mnafahamu hilo,," alisema

No comments:

Post a Comment