Na Eliasa
Ally, Iringa
SIKU chache baada ya
Gazeti la Majira kuandika habari ya ukatili wa kutisha dhidi ya mwalimu
anayedaiwa kuwalawiti wanafunzi wanne mkoani Iringa, mtuhumiwa huyo amekamatwa
na yupo katika mikono ya polisi.
Mwalimu huyo
anafundisha katika Shule ya Sekondari Wanging'ombe, iliyopo Wilaya Mpya ya
Wanging'ombe, mkoani Njombe, Bw. Mwasile Cletus (31).Miongoni mwa wanafunzi waliofanyiwa kitendo hicho mmoja ana miaka10(jina linahifadhiwa),ambaye anasoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Chemchem, mjini humo.
Akizungumza na Majira
jana, Kamanda wa Polisi mkoani Iringa,Ramadhan Mungi ,alisema mtuhumiwa
huyo alikamatwa Septemba 13 mwaka huu, saa 10 jioni, akiwa kwenye nyumba
aliyokuwa akiishi eneo la Don Bosco, mjini humo jirani na Chuo cha Mkwawa
ambako anasoma.
"Mtuhumiwa ni
mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza katika Chuo cha
Mkwawa, anatuhumiwa kuwalawiti wanafunzi wanne baada ya kuwadanganya kuwa
atawapa sh. 200 kila mmoja ili wasitoe siri hiyo kwa wazazi wao," alisema.
Alisema mwanafunzi
mmoja wapo kati ya waliolawitiwa, ndiye aliyewaongoza polisi hadi nyumbani
kwa mshtakiwa na kuwaonesha chumba walichofanyiwa kitendo hicho .
Aliongezakuwa,upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na jalada lake limetumwa kwa Mwanasheria Mkuu w
a Serikali ili kutoa uamuzi kama mtuhumiwa huyo afikishwe mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili za kuwalawiti wanafunzi.
Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti,baadhi ya wakazi wa eneo la DonBosco, Kata ya Mkwawa, walisema kama itabainika mtuhumiwa alifanya vitendo hivyo ,atakuwa ameidhalilisha taaluma y a ualimu ambayo inaheshimika duniani kote.
Baadhi ya Wahadhiri wa chuo hicho ambapo hawakutaka majina yao yaandikwe gazetini,
walisema kuwa mwanafunzi wao atashindwa kuendelea na masomo chuoni hapo.
No comments:
Post a Comment