18 September 2013

MAKAHABA KIZIMBANINa Jazila Mrutu
WANAWAKE watano wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Jiji Sokoine Drive, Dar es Salaam kwa tuhuma za kukutwa wakifanya biashara ya kuuza miili yao.
Mwendesha Mashtaka wa mahakama hiyo, Chrispine Ruiza mbele ya Hakimu Mkazi William Mtaki alisema, Septemba 11, mwaka huu watuhumiwa walikutwa katika maeneo ya Kinondoni jijini humo wakitenda kosa hilo.
Hata hivyo, Ruiza aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Atupele Abraham (22), Anameng Paul (20), Ashura Saidi (23), Elizabeth Philipo (24), Jenifer Enock (20) pamoja na Zabibu Rashidi (24).
Aidha, watuhumiwa hao walikiri kosa ambapo Jenifer Enock atarudishwa kwao mkoani Tabora na wenzake kesi yao itatajwa tena Septemba 23, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment