Na Pamela Mollel, Arusha
SHULE ya Sekondari
Iliboru, iliyopo Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, imefungwa na Serikali kwa
muda usiojulikana baada ya kuwepo kwa hofu ya kuchomwa moto.Chanzo chetu cha
habari kilisema kuwa, tangazo la kufungwa shule hiyo lilitolewa jana asubuhi na
Mkuu wa shule hiyo, Bw.Julius Shila baada ya kushauriana na Bodi ya Shule hiyo.
Akizungumza na Majira
kwa njia ya simu jana, Bw. Shila alikiri shule hiyo kufungwa kwa muda
usiojulikana ambapo uamuzi wa kuifungua utatolewa na Ofisi ya Mkoa wa Arusha."Ni kweli shule imefungwa kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu ambapo wanafunzi
wote wamerejea nyumbani, kuna taratibu ambazo wanapaswa kuzifuata," alisema
Bw. Shila.Baada
ya tangazo la kufungwa kwa shule hiyo, inadaiwa zaidi ya wanafunzi 800
kuanzia kidato cha kwanza hadi sita, wameathirika wakiwemo wanaofanya mitihani
ya mwisho.
No comments:
Post a Comment