- KESI ILIFUNGULIWA 2000 HUKUMU YATOKA 2013
Na Veronica Modest, Serengeti
HALMASHAURI ya Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara, imeshinda kesi
iliyofunguliwa na mkazi wa Kijiji cha Nyamakobiti, wilayani humo, Bw. Charari
Chacha, akipinga halmashauri hiyo kuuza kuku wake kwa gharama ya sh. 1,000
baada ya kukataa kulipa mchango wa ujenzi wa Shule ya Msingi Nyamakobiti.
Akizungumza mwishoni mwa wiki kwenye
Kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo, Mkurugenzi Mtendaji, Bi.
Goody Pamba, alisema kesi hiyo ilifunguliwa mwaka 2000 na hukumu kutolewa
katika Mahakama ya Rufaa jijini Mwanza.
Alisema Bw. Chacha alifungua kesi hiyo
namba 46.2008 baada ya kushindwa katika kesi ya awali namba 18/2000
aliyoifungua katika Mahakama ya Mkoa.Aliongeza kuwa, Mahakama ya Rufaa jijini
Mwanza, ilitoa hukumu Septemba 3 mwaka huu, ambapo Bw. Chacha, alishindwa tena
kwa mara ya pili.
Bi. Pamba alisema, hadi sasa gharama
zilizotumika kuendesha kesi hiyo tangu mwaka 2000 hazijafahamika.Diwani wa kata hiyo, Bw. Rashidi
Mugare, alisema kuanzia mwaka 2000-2013, maendeleo y a kijiji hicho yalirudi
nyuma kutokana na wananchi kutochangia shughuli za maendeleo.
“Kila mtu alipotakiwa kuchangia
shughuli za maendeleo, alitishia kwenda mahakamani kama alivyofanya Bw. Chacha,
wachache ndio waliokubali kuchangia.“ B a a d a y e B w. C h a c h a
alimkomboa kuku wake kwa gharama ya sh. 1,000, hadi sasa kijiji chetu ni cha
mwisho katika suala zima la maendeleo kulingana na sumu iliyomwagwa, kimsingi
kesi hii ilikwamisha mambo mengi ya maendeleo,” alisema.
Alitoa wito kwa wananchi wa kijiji
hicho, kuchangia maendeleo ya elimu ambayo ndio dira ya maisha badala ya
kuendeleza malumbano na kufungua kesi mahakamani.Aliwataka wasijiingize kwenye gharama wasizoweza kuzimudu kwa
kufungua kesi ambazo hazina tija yoyote kwani suala la maendeleo ni kwa faida
ya wananchi, Taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment