Na Goodluck
Hongo
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bw. Bernard Membe, amesema kamwe Tanzania haiwezi kutengwa na nchi
za Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC).Alisema
Tanzania ina rasilimali za kutosha kama bandari, barabara nzuri, chakula cha
kutosha ambazo ni vigumu kwa nchi hizo kuchukua uamuzi huo
.Bw.
Membe aliyasema hayo Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari
Dar es Salaam jana.Akizungumzia mkutano
wa Viongozi wa Maziwa Makuu uliofanyika juzi nchini Uganda, Bw. Membe alisema
wakuu hao wametia siku 17 kwa waasi wa M23 na Serikali ya Congo (DRC), kumaliza
mgogoro wao.
Kama mgogoro huo
hautapatiwa ufumbuzi ndani ya siku hizo, viongozi hao watakutana tena na
kujadili hatua za kuchukua."Wa k u u w a n
c h i h i z i wamekubaliana kutoa siku 17 kwa waasi wa M23 na Serikali ya DRC
ili wamalize mgogoro wao, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ataendela kuwa
msuluhishi wa mgogoro huo na nchi zote za Maziwa Makuu," alisema Bw.
Membe.
Aliongeza kuwa,
mazungumzo kati ya Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Rwanda, Paul Kagame,
yalifanyika kwa mafanikio makubwa na yalichukua zaidi ya saa moja kila mmoja
akitoa la moyoni ambapo kinachotarajiwa kutokea kwa siku zijazo ni kuona
mikutano ya viongozi wa nchi hizo inafanyika katika nchi ya Rwanda na Tanzania
ili kuimarisha uhusiano.
Bw. Membe alisema,
kuhusu mgogoro wa Tanzania na Malawi kuhusu Ziwa Nyasa, alisema hadi sasa kuna
jopo la wataalamu wa sheria nchini, lipo nchini humo wakifanya mazungumzo.
Akizungumzia Uchaguzi Mkuu nchini Madagascar unaotarajiwa kufanyika
Oktoba mosi mwaka huu, kutakuwa na wagombea 33 wa nafasi ya urais na kama
mshindi hatapatikana kutokana na wingi wa wagombea hao, utarudiwa tena Oktoba
20,2013.
No comments:
Post a Comment