- SASA HASIRA ZAO KUMALIZIA KWA RUVU SHOOTING J'MOSI
Na Elizabeth Mayemba
Kocha Mkuu wa Yanga, Ernest Brandts
amesema kuwa umakini mdogo wa mabeki wake ndio uliowafanya wapoteze mchezo wa
juzi dhidi ya Azam FC ,baada ya kufungwa mabao 3-2 mechi iliyochezwa Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumz a Da r e s Salaam jana, Brandts alisema katika mchezo huo timu yake
ilicheza vizuri dakika zote 90, lakini kukosa umakini ndio kulisababisha
matokeo yaishe vile.
"Wachezaji
wangu walicheza vizuri dakika zote 90, lakini Azam FC walitumia kasoro yetu
kidogo na kuondoka na ushindi katika mchezo huo, hivyo wachezaji wangu
wanatakiwa kujipanga upya," alisema Brandts.
Alisema sasa
hivi anaangalia mechi ijayo dhidi ya Ruvu Shooting itakayochezwa J umamosi ijayo , hivyo watahakikisha wanaondoka na pointi zote tatu ili kujiweka
katika mazingira mazuri katika kampeni zao za kutetea ubingwa wao.
Kocha huyo alisema mechi na Azam
imeshakwisha sasa wanachotakiwa kuangalia ni mechi inayokuja, hivyo wachezaji
wake wanatakiwa kurekebisha kasoro zilizopita ili wapate ushindi mechi ijayo.
Ukiacha mabeki, pia kocha huyo amelia
na safu yake ya ushambuliaji kuwa walipata nafasi nyingi za kufunga lakini
walishindwa kufanya hivyo na kuwataka wajirekebishe mechi ijayo.
Kwa upande wa kocha wa Azam FC Stewart
Hall alisema kuwa, wapinzani wao Yanga waliwazidi kila idara na wao wameshindia
bahati tu. "Ile mechi Yanga ndio waliostahili ushindi lakini wachezaji
wangu walitumia makosa kidogo yaliyofanywa na wachezaji wa Yanga na wao kufunga
mabao," alisema Hall.
No comments:
Post a Comment