Na Mwandishi Wetu
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
kati ya wenyeji Azam FC na Yanga lililochezwa juzi katika Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam, limeingiza sh. 138,188,000
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema watazamaji
waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 33 la VPL msimu wa 2013/14
lililomalizika kwa Azam kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 walikuwa 24,020
. Alisema viingilio katika mechi hiyo
vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata
mgawo wa sh. 33,065,409.1 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa
ni sh. 21,079,525.42.
"Mgawo mwingine wa mapato hayo ni
asilimia 15 ya uwanja sh. 16,812,919.89, tiketi sh. 5,022,342, gharama za mechi
sh. 10,087,751.93, Kamati ya Ligi sh. 10,087,751.93, Mfuko wa Maendeleo ya
Mpira wa Miguu (FDF) sh. 5,043,875.97 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar
es Salaam (DRFA) sh. 3,923,014.64," alisema Wambura.
Alisema mechi iliyopita ya VPL kwenye
uwanja huo kati ya Simba na Mbeya City iliingiza sh. 123,971,000.
Wakati huo huo, mechi
namba 12 ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati ya Toto Africans na Polisi Dodoma
iliyokuwa ichezwe Jumamosi ijayo Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza imesogezwa
mbele kwa siku moja.
Timu hizo za kundi C sasa zitapambana
Jumapili kwenye uwanja huo huo ili kupisha mechi namba 10 kati ya Pamba na
Stand United FC ya Shinyanga itakayochezwa Jumamosi (Septemba 28 mwaka huu).
Mechi nyingine za kundi hilo
zitakazochezwa Jumamosi ni Mwadui na Polisi Tabora (Uwanja wa Kambarage,
Shinyanga) wakati Kanembwa JKT na Polisi Mara zitacheza kwenye Uwanja wa Lake
Tanganyika mjini Kigom
No comments:
Post a Comment