Na
Mwandishi Wetu
Mchungaji Ambilikile Mwaisapila
(Babu wa Kikombe) wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), amesema
Mungu ameendelea kujifunua kwake na kumuonesha kuwa Tanzania itakuwa kioo cha
Afrika na dunia kwa ujumla.
Alitoa kauli
hiyo juzi mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akizungumza na wakazi wa
kijiji cha Samunge, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakati msafara wa Waziri
Mkuu uliposimama nyumbani kwake ili kumsalimia akiwa njiani kurejea mjini
Arusha.
Mchungaji
Mstaafu Mwaisapila alisema kuna mambo mengi ambayo yameandikwa kwenye Biblia,
lakini hayakutokea Israeli na sasa yatafanyika hapa Samunge.
“Mungu
ametupenda sana, yanakuja mambo makubwa na wala hayako mbali. Kama mimi ni mzee
na nitayaona, kwa hiyo mtarajie kuwa hayako mbali kutokea,” alisema huku
akishangiliwa na wananchi.
Alisema katika
mafunuo aliyopewa na Mungu ameoneshwa kwamba watu wengi zaidi watafurika
kijijini Samunge kuliko ilivyokuwa hapo awali. Alitumia fursa hiyo kuishukuru
Serikali kwa misaada iliyotoa wakati wa kugawa kikombe ikiwemo mahema, maji na
ulinzi.
Waziri Mkuu,
Pinda ambaye yuko mkoani Arusha kwa ziara maalum ya kusikiliza matatizo na
migogoro ya ardhi yanayowakabili wakazi wa wilaya ya Ngorongoro, katika tarafa
za Ngorongoro, Loliondo na Sale alisema anakubaliana na utabiri wa Mch.
Mwaisapila kwani Tanzania imejaliwa gesi nyingi na mafuta mengi ambavyo
vitabadili sura ya Taifa hili.
"Mungu
ametupa gesi nyingi sana, katika miaka miwili tutakuwa na umeme kila mahali.
Tuna makaa ya mawe ambayo ni nishati kubwa na sasa tuna fursa ya kupata nishati
ya umeme kutoka ardhini (Geo-thermal) katika Ziwa Natron," alisema.
Alisema
Tanzania imekuwa kimbilio la kila mwekezaji na sababu kubwa ni amani na utulivu
uliopo nchini. Aliwaeleza wakazi wa Samunge kwamba mapema mwakani mkandarasi wa
barabara atakuwa katika eneo lao kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya lami ambapo
awamu ya kwanza itaanzia Wasso hadi Mto wa Mbu kupitia Samunge.
Akitoa ombi maalum kwa niaba ya vijana
mbele ya Waziri Mkuu, Elias Kalumbwa, alisema wanaomba kuchimbiwa bwawa ili
waweze kujiajiri kupitia kilimo cha mboga na matunda.Kalumbwa ambaye amesomea masuala ya
wanyamapori alisema eneo la kuchimba bwawa lipo katika mto wa msimu unaopita
kijijini hapo.
Naye MarthaSereri (70) alimweleza
Waziri Mkuu kwamba wanaomba jimbo la Ngorongoro ligawanywe kwa sababu ni kubwa
sana kiasi kwamba inamuwia vigumu mbunge wao kufika maeneo yote. Aliomba pia
wapatiwe walimu wa sayansi na hisabati kwa ajili ya shule 10 za sekondari zilizopo
kwenye tarafa yao.
Aliomba wapatiwe mikopo ya matreka ili
waweze kuongeza ukubwa wa mashamba yao. “Tunaomba mikopo ya matrekta na plau,
haya mashamba umeyaona njiani yamelimwa na Wakenya. Ukikodisha trekta kila
ekari unatozwa sh. 100,000/-. Je tutafika wapi? Mkitukopesha matrekta mtakuwa
mmetusaidia zaidi,” alisema.
Akijibu hoja hizo, Waziri Mkuu alisema
hoja zao ni za msingi na kwamba suala la vijana kupatiwa bwawa ni jambo
linalowezekana kupitia mipango ya maendeleo ya kilimo ya wilaya (DADPS).
"Andaeni andiko lenu, inabidi
litoke kwa wananchi na si Serikalini. Mkituletea ni jambo linalowezekana kwani
liko ndani ya mipango ya wilaya," alisema.
Akijibu hoja kuhusu ukubwa wa jimbo,
Waziri Mkuu aliwaambia wakazi hao kwamba inawezekana kuongeza jimbo isiwe
suluhisho la matatizo yao kwa sababu ya jiografia ya eneo lao.
"Kuongeza jimbo inaweza isiwe jibu
la kila kitu kwani matatizo mnayopata yanatokana na jiografia ya eneo lenu,
kutoka Ngorongoro, Loliondo hadi huku Sale.
Mimi
nadhani tuangalie pia uwezekano wa kuwapa Halmashauri ili kusogeza huduma kwa
wananchi. Tutaangalia njia zote mbili na kuona ipi italeta majibu ya haraka
kwenu," alisema.
mchungaji.na.usanii
ReplyDeleteSiyo msanii, ni mjasiriamali.
DeleteZimepungua, anasaka zingine tena!
ReplyDeleteZimepungua, anasaka zingine tena!
ReplyDeletehuyu babu amezidi sana.anatakiwa kuchunguzwa
ReplyDeleteviongozi kuweni makini sana na wajanja kama hao
ReplyDeleteHivi ni watu wangapi wameshapoteza maisha hapo walipoacha dozi za hospitali na kuki-nywea kikombe? Yaani PM anakwenda kumwona mtu kama huyo eti "amepitia akiwa safarini" hii ni kitu chaajabu sana ...kwanini PM haoni kuwa hii inatoa endorsement kwa huduma ya mtu huyo......sijui viongozi wetu hawana washauri!
ReplyDeleteFor this time watanzania wameng'amuka juu ya babu huyo. Mara kadhaa amejaribu kuzungumza juu ya ndoto zake zingine lakini hakuna aliyeshawishika nae. time has gone.
ReplyDeletedu inabidi tuwe makini hata bibble inasema watu wangu wataangamia kwa kukosa maarifa
ReplyDeleteUnajua tatizo ninini? Watu wengi wanayo matatizo mengi, hivyo wanaangaika kutafuta msaada; na kwa sababu hawamjui Mungu wa kweli asiyeshindwa na lolote na kwenda kwake ndiyo maana utawakuta wanahangaika kutafuta njia zingine kama kwenda kwa babu n.k. Hivyo napenda kuwashauri watu wa jinsi hiyo wamuelekee Mungu maana ndiye anayesema "NIITE NAMI NITAKUITIKIA... NJOONI KWANGU NYINYI NYOTE MSUMBUKAO NAKULEMEWA NA MIZIGO NAMI NITAWAPUMZISHA...MIMI NDIYE NIKUPONYAYE... KWA KUPIGWA KWAKE NANYI MLIPONYWA..."
ReplyDeletealishakosea toka mwanzoni. Iweje dawa yenye upako wa Mungu ichemshwe na yeyote yule hata kama jana alizini/kuiba n.k. na bado ifanye kazi? Angekua anachimba dawa mwenyewe, anachemsha menyewe na kugawa basi mimi ningeamini kwa kuwa namwamini. Lakini watu lukuki wanaishughulia? Mimi hapana kwa hapo.
ReplyDeleteIla kwa sasa kama watu ni wachache kama 10 nakushuka kwa siku naweza kwenda kumsikiliza
akija dajal ndio atasomba watu wote
ReplyDeleteHuyo babu ni mjasiriamali na mbunifu mzuri wa biashara. Maana biashara ni ubunifu na ukiweza kubuni kitu kipya hapo una-win!!!!!!!!!!!
ReplyDeletehe is creative,he thinks how to make money,lets not complaining about ambilikile,i think it will good to turn back our eyes and combating with negligence,who keep ripping the govt resources
DeleteDu! haya majanga, kiukweli huo ni ujanja wa nyani kula maindi mabichi.kwanini hapewi tuzo ya kuwa msanii bora wa mwaka ikiwezekana wa karne?
ReplyDeleteKuna roho za aina tatu zenye uwezo wa kufunua mambo na kudai ni mafunuo kutoka kwa Mungu Zijaribuni hizo roho kwa neno la Mungu. Kuna Roho Mtakatifu,roho wa mwanadamu na roho wa shetani . Angalieni msije mkatumika katika roho ya mwanadamu ama ya shetani kwa sababu ya kutaka jibu la haraka.
ReplyDeletenapita
ReplyDeleteKinachotakiwa ni wewe mwenye matatizo kutengeneza mambo yako na Mungu ambaye ndiye mweza wa yote. Ukishajiunganisha na Mungu huna haja ya kunywa kikombe kwani Mungu atalituma neno nalo litafanya uponyaji Zab.107:20. Hivyo mtafuteni kwanza huyo Mungu anayeweza ndipo mpate uponyaji wenu - Soma kitabu cha Yeremia
ReplyDeletedu huyo babu naona sasa kaiteka nchi mpaka pm anamtembelea ila kumbukeni kwamba hz ni nyakati za mwisho asema bwana, watu wangu wanakosa maarifa asema bwana be care all Taanzanian babu anataka kuiteka nci
ReplyDeleteKuna aina nyingi za vichaa,huyu babu ni babu ni mmoja wa watu wenye vichaa hatari sana....Aogopwe kama UKOMA!
ReplyDeleteBabu amenikera sana.Amesababisha vifo vya watu went.Sijui kwa nini asichukuliwe hatua
ReplyDeleteAmelaaniwa mtu yule amtegemeae mwanadamu,Biblia inasema nini kuhusu uponyaji? Tukitaka majibu ya haraka mambo ndo yanakuwa hivyo,utapeli mtupu.
ReplyDeleteKila mtu hula tokana na urefu wa kamba yake. Mwacheni Babu naye ale kwani mnalazimishwa kwenda kwake??
ReplyDeletePm alikwenda kujikumbushia kwani ni miongoni mwa waliobwia kikombe zama zile!!
ReplyDeletehahahah,babu anataka tena audanganye uma
ReplyDeleteHaya PM kwa ku'renew' babu unadanganya hata vgogo! we hatari!
ReplyDeletebabu hana mpya, anatafuta namna ya kuwafanya watanzania wamwamini tena, amepotea, mwizi ukiiba ukatajirika acha maanaukirudia unaweza ukaangukia pua, nafikiri hata pm alienda kumshangaa tu kwa usanii wake
ReplyDelete