26 September 2013

BABU WA KIKOMBE LOLIONDO AIBUKA Na Mwandishi Wetu
  Mchungaji Ambilikile Mwaisapila (Babu wa Kikombe) wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), amesema Mungu ameendelea kujifunua kwake na kumuonesha kuwa Tanzania itakuwa kioo cha Afrika na dunia kwa ujumla.

Alitoa kauli hiyo juzi mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Samunge, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakati msafara wa Waziri Mkuu uliposimama nyumbani kwake ili kumsalimia akiwa njiani kurejea mjini Arusha.
Mchungaji Mstaafu Mwaisapila alisema kuna mambo mengi ambayo yameandikwa kwenye Biblia, lakini hayakutokea Israeli na sasa yatafanyika hapa Samunge.
“Mungu ametupenda sana, yanakuja mambo makubwa na wala hayako mbali. Kama mimi ni mzee na nitayaona, kwa hiyo mtarajie kuwa hayako mbali kutokea,” alisema huku akishangiliwa na wananchi.
Alisema katika mafunuo aliyopewa na Mungu ameoneshwa kwamba watu wengi zaidi watafurika kijijini Samunge kuliko ilivyokuwa hapo awali. Alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa misaada iliyotoa wakati wa kugawa kikombe ikiwemo mahema, maji na ulinzi.
Waziri Mkuu, Pinda ambaye yuko mkoani Arusha kwa ziara maalum ya kusikiliza matatizo na migogoro ya ardhi yanayowakabili wakazi wa wilaya ya Ngorongoro, katika tarafa za Ngorongoro, Loliondo na Sale alisema anakubaliana na utabiri wa Mch. Mwaisapila kwani Tanzania imejaliwa gesi nyingi na mafuta mengi ambavyo vitabadili sura ya Taifa hili.
"Mungu ametupa gesi nyingi sana, katika miaka miwili tutakuwa na umeme kila mahali. Tuna makaa ya mawe ambayo ni nishati kubwa na sasa tuna fursa ya kupata nishati ya umeme kutoka ardhini (Geo-thermal) katika Ziwa Natron," alisema.
Alisema Tanzania imekuwa kimbilio la kila mwekezaji na sababu kubwa ni amani na utulivu uliopo nchini. Aliwaeleza wakazi wa Samunge kwamba mapema mwakani mkandarasi wa barabara atakuwa katika eneo lao kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya lami ambapo awamu ya kwanza itaanzia Wasso hadi Mto wa Mbu kupitia Samunge.
  Akitoa ombi maalum kwa niaba ya vijana mbele ya Waziri Mkuu, Elias Kalumbwa, alisema wanaomba kuchimbiwa bwawa ili waweze kujiajiri kupitia kilimo cha mboga na matunda.Kalumbwa ambaye amesomea masuala ya wanyamapori alisema eneo la kuchimba bwawa lipo katika mto wa msimu unaopita kijijini hapo.
  Naye MarthaSereri (70) alimweleza Waziri Mkuu kwamba wanaomba jimbo la Ngorongoro ligawanywe kwa sababu ni kubwa sana kiasi kwamba inamuwia vigumu mbunge wao kufika maeneo yote. Aliomba pia wapatiwe walimu wa sayansi na hisabati kwa ajili ya shule 10 za sekondari zilizopo kwenye tarafa yao.
  Aliomba wapatiwe mikopo ya matreka ili waweze kuongeza ukubwa wa mashamba yao. “Tunaomba mikopo ya matrekta na plau, haya mashamba umeyaona njiani yamelimwa na Wakenya. Ukikodisha trekta kila ekari unatozwa sh. 100,000/-. Je tutafika wapi? Mkitukopesha matrekta mtakuwa mmetusaidia zaidi,” alisema.
  Akijibu hoja hizo, Waziri Mkuu alisema hoja zao ni za msingi na kwamba suala la vijana kupatiwa bwawa ni jambo linalowezekana kupitia mipango ya maendeleo ya kilimo ya wilaya (DADPS).
"Andaeni andiko lenu, inabidi litoke kwa wananchi na si Serikalini. Mkituletea ni jambo linalowezekana kwani liko ndani ya mipango ya wilaya," alisema.
  Akijibu hoja kuhusu ukubwa wa jimbo, Waziri Mkuu aliwaambia wakazi hao kwamba inawezekana kuongeza jimbo isiwe suluhisho la matatizo yao kwa sababu ya jiografia ya eneo lao.
"Kuongeza jimbo inaweza isiwe jibu la kila kitu kwani matatizo mnayopata yanatokana na jiografia ya eneo lenu, kutoka Ngorongoro, Loliondo hadi huku Sale.
Mimi nadhani tuangalie pia uwezekano wa kuwapa Halmashauri ili kusogeza huduma kwa wananchi. Tutaangalia njia zote mbili na kuona ipi italeta majibu ya haraka kwenu," alisema.

28 comments:

 1. mchungaji.na.usanii

  ReplyDelete
 2. Zimepungua, anasaka zingine tena!

  ReplyDelete
 3. Zimepungua, anasaka zingine tena!

  ReplyDelete
 4. huyu babu amezidi sana.anatakiwa kuchunguzwa

  ReplyDelete
 5. viongozi kuweni makini sana na wajanja kama hao

  ReplyDelete
 6. Hivi ni watu wangapi wameshapoteza maisha hapo walipoacha dozi za hospitali na kuki-nywea kikombe? Yaani PM anakwenda kumwona mtu kama huyo eti "amepitia akiwa safarini" hii ni kitu chaajabu sana ...kwanini PM haoni kuwa hii inatoa endorsement kwa huduma ya mtu huyo......sijui viongozi wetu hawana washauri!

  ReplyDelete
 7. For this time watanzania wameng'amuka juu ya babu huyo. Mara kadhaa amejaribu kuzungumza juu ya ndoto zake zingine lakini hakuna aliyeshawishika nae. time has gone.

  ReplyDelete
 8. du inabidi tuwe makini hata bibble inasema watu wangu wataangamia kwa kukosa maarifa

  ReplyDelete
 9. Unajua tatizo ninini? Watu wengi wanayo matatizo mengi, hivyo wanaangaika kutafuta msaada; na kwa sababu hawamjui Mungu wa kweli asiyeshindwa na lolote na kwenda kwake ndiyo maana utawakuta wanahangaika kutafuta njia zingine kama kwenda kwa babu n.k. Hivyo napenda kuwashauri watu wa jinsi hiyo wamuelekee Mungu maana ndiye anayesema "NIITE NAMI NITAKUITIKIA... NJOONI KWANGU NYINYI NYOTE MSUMBUKAO NAKULEMEWA NA MIZIGO NAMI NITAWAPUMZISHA...MIMI NDIYE NIKUPONYAYE... KWA KUPIGWA KWAKE NANYI MLIPONYWA..."

  ReplyDelete
 10. alishakosea toka mwanzoni. Iweje dawa yenye upako wa Mungu ichemshwe na yeyote yule hata kama jana alizini/kuiba n.k. na bado ifanye kazi? Angekua anachimba dawa mwenyewe, anachemsha menyewe na kugawa basi mimi ningeamini kwa kuwa namwamini. Lakini watu lukuki wanaishughulia? Mimi hapana kwa hapo.
  Ila kwa sasa kama watu ni wachache kama 10 nakushuka kwa siku naweza kwenda kumsikiliza

  ReplyDelete
 11. akija dajal ndio atasomba watu wote

  ReplyDelete
 12. Huyo babu ni mjasiriamali na mbunifu mzuri wa biashara. Maana biashara ni ubunifu na ukiweza kubuni kitu kipya hapo una-win!!!!!!!!!!!

  ReplyDelete
  Replies
  1. he is creative,he thinks how to make money,lets not complaining about ambilikile,i think it will good to turn back our eyes and combating with negligence,who keep ripping the govt resources

   Delete
 13. Du! haya majanga, kiukweli huo ni ujanja wa nyani kula maindi mabichi.kwanini hapewi tuzo ya kuwa msanii bora wa mwaka ikiwezekana wa karne?

  ReplyDelete
 14. Kuna roho za aina tatu zenye uwezo wa kufunua mambo na kudai ni mafunuo kutoka kwa Mungu Zijaribuni hizo roho kwa neno la Mungu. Kuna Roho Mtakatifu,roho wa mwanadamu na roho wa shetani . Angalieni msije mkatumika katika roho ya mwanadamu ama ya shetani kwa sababu ya kutaka jibu la haraka.

  ReplyDelete
 15. Kinachotakiwa ni wewe mwenye matatizo kutengeneza mambo yako na Mungu ambaye ndiye mweza wa yote. Ukishajiunganisha na Mungu huna haja ya kunywa kikombe kwani Mungu atalituma neno nalo litafanya uponyaji Zab.107:20. Hivyo mtafuteni kwanza huyo Mungu anayeweza ndipo mpate uponyaji wenu - Soma kitabu cha Yeremia

  ReplyDelete
 16. du huyo babu naona sasa kaiteka nchi mpaka pm anamtembelea ila kumbukeni kwamba hz ni nyakati za mwisho asema bwana, watu wangu wanakosa maarifa asema bwana be care all Taanzanian babu anataka kuiteka nci

  ReplyDelete
 17. Kuna aina nyingi za vichaa,huyu babu ni babu ni mmoja wa watu wenye vichaa hatari sana....Aogopwe kama UKOMA!

  ReplyDelete
 18. Babu amenikera sana.Amesababisha vifo vya watu went.Sijui kwa nini asichukuliwe hatua

  ReplyDelete
 19. Amelaaniwa mtu yule amtegemeae mwanadamu,Biblia inasema nini kuhusu uponyaji? Tukitaka majibu ya haraka mambo ndo yanakuwa hivyo,utapeli mtupu.

  ReplyDelete
 20. Kila mtu hula tokana na urefu wa kamba yake. Mwacheni Babu naye ale kwani mnalazimishwa kwenda kwake??

  ReplyDelete
 21. Pm alikwenda kujikumbushia kwani ni miongoni mwa waliobwia kikombe zama zile!!  ReplyDelete
 22. hahahah,babu anataka tena audanganye uma

  ReplyDelete
 23. Haya PM kwa ku'renew' babu unadanganya hata vgogo! we hatari!

  ReplyDelete
 24. babu hana mpya, anatafuta namna ya kuwafanya watanzania wamwamini tena, amepotea, mwizi ukiiba ukatajirika acha maanaukirudia unaweza ukaangukia pua, nafikiri hata pm alienda kumshangaa tu kwa usanii wake

  ReplyDelete