19 September 2013

AIRTEL, TRA KUWEZESHA WATEJA



Na Frank Monyo
AIRTEL Tanzania kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) wamezindua rasmi huduma ya kufanya malipo ya ada za leseni za magari kupitia huduma ya Airtel money.Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wa teja Airtel Adriana Lyamba, alisema huduma ya kulipia leseni ya magari kupitia Airtel m oney imeleta unafuu kwa wateja watakaotaka kulipia leseni za magar ambapo hupatikana bure kwa wateja wote wa Airtel nchi nzima
.Mkurugenzi huyo alisema kuwa huu ni mwendelezo wa mapinduzi ya huduma za kifedha kupitia hudum a ya Airtel money inayomuhakikishia mteja uharaka,unafuu, usalama na urahisi zaidi katika kulipia huduma mbalimbali.
Akizungumzia kuhusu huduma ya malipo ya ada za leseni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Malipo ya Kodi na Elimu TRA Diana Masalla alisema huduma hii mpya inahusisha malipo ya ada za leseni za mag ari, ada za uhamisho wa magari pamoja na malipo mengine ya ada za usajili wa magari.Huduma hii itawezesha ukusanyaji wa malipo ya ada/kodi zifanyike kwa njia rahisi na nafuu.Unawezaku pata kiasi cha kulipia ada unayotakiwa kulipia kisha ukalipia hapohapo ndani ya sekunde chache kupitia huduma ya Airtel money.
Meneja wa kitengo cha Airtel money John Ndunguru alisema, huduma hii inapatikana kw a wateja wa malipo ya awali na ya mwezi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hii ,Airtel imeweza kuiweka MENU ya Airtel Money“ TRA MAGARI” ili kuweza kurahisisha ulipaji wa ada na kuiwezesha serikali kukusanya ada kwa gharama nafuu zaidi”
Kwa upande wake Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, ASP Mohamed Mpinga alisema“Ninawa pongeza sana kampuni ya Airtel kupitia huduma yake ya Airtel Money kwa kushirikiana na Mamlaka y a MapatoTanzania(TRA )kurahisisha ukusanyaji wa kodi hii ya Ada za magari maarufu kama Road License.
“Hii ni huduma nzuri inayosaidia Watanzania kuokoa muda wao pale wanapoweza kutumia simu zao kup itia mtandao wa Airtel kulipia ada ya magari yao kila mwaka bila usumbufu.
Naomba niwakumbushe kuwa wiki ya usalama barabarani itaanza wiki ijayo tarehe 23.9.2013 hivyo ma mbo yote ya ukaguzi wastika za ada za magari yaani ( Road Licence) pamoja na stika za usalama barabarani na ukaguzi wa vyombo vyote vya moto utaenda sambamba, hivyo ninawak umbusha watumiaji wote wa vyombo vyote vya moto kufuata sheria zote .

No comments:

Post a Comment