19 September 2013

WATANZANIA KUANZA KUNUFAIKA NA MAKAA


Jazila Mrutu na Revina John
TANZANIA inategemea kushika nafasi ya nne katika uzalishaji wa chuma pamoja na uchimbaji wa
makaa ya mawe kupitia mradi unaotegemewa kuanzishwa mwezi Mei, mwakani katika eneo la Liganga na
Mchuchuma wilayani Ludewa
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Shirika la Taifa na Maendeleo (NDC), Abel Ngapemba alisema Tanzania itakuwa ya nne ikifuatiwa na Afrika Kusini katika uchimbaji wa madini hayo ambapo itazalisha tani milioni 8.5 kwa mwaka. 
  Hata hivyo alisema kuwa, mbali na uzalishaji wa chuma madini mengine yatakayotokana na mgodi huo ni Titanium tani 175,400 na Vanadium tani 5,000 kwa mwaka. “Katika uzalishaji huu madini aina ya Titanium yatasaidia katika uzalishaji wa vyuma imara ambavyo mara nyingi vinatumika katika utengenezaji wa injini za ndege, ambapo Afrika Kusini na Amerika wamekuwa wakiizalisha kwa wingi,” alisema Ngapemba
Aidha, mradi huu ni moja ya miradi miwili iliyopo katika mkataba kati ya NDC na Shirika la Sichuan Hongda Group (SHG) ya uzalishwaji wa mgodi wa makaa ya mawe na ujenzi wa kituo cha kufua umeme megawati 600 katika eneo la Mchuchuma pamoja na ujenzi wa msongo wa umeme kilowati 220 kwa Mchuchuma na Liganga

1 comment:

  1. Tunakaribisha mradi wa Liganga kwa utoaji wa chuma na huo wa Ludewa kwa makaa ya mawe.

    Tanzania ikitumia vizuri miradi hii itakuwa ni nchi ya kujivunia sana duniani kwani ujenzi wa Taifa lolote linahitaji miundo mbinu kama Barabara ambazo nyingi zinahitaji vyuma imara kwenye madaraja yake.

    Ukiangalia sana barabara zetu ni nyembamba na sehemu ya madaraja utakuta sehemu nyingine ni ya kupita gari moja tu kwa wakati kama daraja la wami nk.

    Aidha sehemu nyingi za vivuko zimeshindikana kujengwa kwa ukosefu wa vyuma kama vivuko vya Kilombero, Busisi,nk

    Kupatikana kwa vyuma kutaharakisha hata barabara za juu flyovers ambazo hupunguza sana msongomano mijini.Aidha majengo yetu yatajengwa kwa viwango vya kimataifa sasa kwani kama tatizo lilikuwa ni vyuma na kusababisha magorofa kuanguka sasa hali hiyo itakuwa ahuweni kwani mali ghafi yatapatikana hapo nyumbani

    Kwa maana hiyo secta ya ujenzi wa barabara na ujenzi wa majumba zinatakiwa kulipokea jambo hili kwa mikono miwili ili kuwezesha uchumi wetu kukua kwa kasi kwani nchi ikishakuwa na barabara nyingi na nzuri zenye madaraja madhubuti usafirishaji wa bidhaa za mashambani na viwandani huongezeka

    Kuongezeka huko hupanua masoko katika baadhi ya sehemu na kujenga miji mipya hasa maeneo mapys ya vijijini.

    Aidha tunalipokea kwa mikono miwili hili la kuzalisha makaa ya mawe siyo tu kwa kupata umeme wa msongo MG 600 kwenye gridi ya Taifa kuongezea na huo wa Mtwara wa MG 1500 hii inaonyesha ni jinsi gani sasa Tanzania itakavyokuwa na umeme mwingi wa kutosheleza matumizi ya nyumbani sasa nyumba mpya zitazojengwa,viwanda vipya sasa na vitakavyojengwa na kuuza nje ya nchi.

    Aidha kuwepo na umeme wa kutosha kutaanzisha soko linguine la uanzishaji wa vyuo vya elimu ya juu wanafunzi wa kujiunga elimu ya juu
    wataongezeka

    Kuongezeka huko kutasabisha kuanzisha sehemu mbalimbali za kufanya majaribio ya mambo makubwa na kujenga viwanda vikubwa kama vya magari mitambo ya kuzalisha vipuli na kadhalika.

    Aidha ni jinsi gani sasa watanzania watakapoanza kutumia makaa ya mawe kwa nishati ndogo ndogo kama kupikia kuyeyusha vyuma katika viwanda vidogo vidogo kutumia makaa kama kwenye viwanda, kuwa vyanzo vya nishati kwenye viwanda kama vya bia, soda cementi na kupunguza utumiaji wa fedha za kigeni katika kuagiza malighafi hizo.

    Ni wakati sasa serikali ya Mheshimiwa Raisi Kikwete kulitazama hili kwa upeo mkubwa na kukomesha mikataba binafsi ambayo haitalifanikisha Taifa na kulinda soko la ajira na kuwepo na uzawa kwanza na upendeleo kwa watanzania kwanza ili kufikia malengo yake na siyo kulididimiza Taifa kwa kuingia mikataba ya kunufaisha mataifa mengine na mali asili hizi

    Mungu ibariki Tanzania ili mali asili hizi zitumiwe kwa faida ya watanzania wa siyo wageni tu

    ReplyDelete