26 August 2013

YANGA,ASHANTI ZAINGIZA MILIONI 102/-



Na Mwandishi Wetu
MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), kati ya Yanga na Ashanti United iliyochezwa juzi katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 102,856,000
.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura, watazamaji 17,744 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba moja ya VPL msimu wa 2013/2014.
Katika mechi hiyo mabingwa watetezi Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Ashanti ambayo imepanda daraja msimu huu.
Alisema viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 24,400,102.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 15,689,898.31.
Wambura alisema mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 12,406,831.75, tiketi sh. 4,453,890, gharama za mechi sh. 7,444,099.05, Kamati ya Ligi sh. 7,444,099.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,722,049.53 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,894,927.41.

No comments:

Post a Comment