Na
Joseph Mwambije, Songea
VIFO vya
samaki katika ziwa Nyasa katika Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, vimezusha hofu
kati ya Tanzania na Malawi kutokana na kila upande kuhisi umetupa fataki ziwani
humo. Hisia hizo zinatokana na pande mbili hizo kuwa kwenye mgogoro wa mpaka.
Kauli hiyo ilitolewa na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dkt.Teresa Huvisa,
akizungumza na wananchi kandoni mwa Ziwa Nyasa wakati wa ziara yake ya siku
tatu mkoani Ruvuma, alisema;“Nimepata taarifa kuwa
samaki wanaokufa katika Ziwa Nyasa sasa wameleta hofu kwa wananchi wa nchi zote
mbili Tanzania na Malawi, kwa hiyo ninachoweza kuwaambia ni kwamba tutatuma
wataalamu kuchunguza chanzo cha samaki kufa,” alisema Dkt. Huvisa.
Lakini pia kuna wavuvi wanatumia majani yanayoitwa
mtunungu kuvulia samaki ambayo ukimwaga ziwani au mtoni samaki wanakufa, kwa
hiyo msitumie sumu kuvulia samaki.
Alisema samaki hao wanakufa ziwani humo bila kujua
chanzo chake msiwale.
Hata hivyo aliwatoa hofu wananchi hao waishio mpakani mwa nchi ya Malawi
na Msumbiji kutokana na mzozo wa kugombea umiliki na mpaka wa ziwa hilo kati ya
Tanzania na Malawi, kutoogopa mzozo huo na kwamba Malawi haina ubavu wa
kupigana na Tanzania endapo nchi hizo zitaingia vitani
No comments:
Post a Comment