Na Rehema Mohamed
WAFUASI
52 wa Shekhe P o n d a I s s a P o n d a , waliohukumiwa adhabu ya kifungo cha
mwaka mmoja jela, wamekata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakipinga
hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyowatia hatiani.
Katika rufaa
yao hiyo, wafungwa hao, kupitia kwa wakili wao, Mohamed Tibanyendela, wanapinga
hukumu ya Mahakama ya Kisutu, ambapo pamoja na mambo mengine, wanadai kuwa
hakimu alikosea kisheria kuchambua ushahidi wa pande zote uliowasilishwa
mahakamani hapo.
Pia wanadai
kuwa katika hukumu hiyo, hakimu alijikanganya kwa kumwachia huru mmoja wa
washtakiwa na kuwatia hatiani washtakiwa wengine.
Ru f a a h i y
o ime p a n gwa kusikilizwa leo na Jaji Salvatory Bongole, mahakamani hapo.
Machi mwaka huu Hakimu Sundi Fimbo wa Mahakama ya Kisutu aliwahukumu washtakiwa
hao wa kesi ya kula njama na kufanya maandamano isivyo halali kwenda jela mwaka
mmoja baada ya kuwatia hatiani katika mkosa yaliyokuwa yakiwakabili.
Washtakiwa hao
walidaiwa kutenda makosa hayo Februari 15, mwaka huu. Washtakiwa katika kesi
hiyo walikuwa ni Salum Makame, Said Idd na Ally Nandumbi, Makame, Idd na
Nandumbi, Hussein Athumani, Seif Rwambo, Abdull Ally, Waziri Swed, Naziru
Waziri, Ahmad Rashid, Jumanne Kayogola, Hamis Tita, Amri Diyaga, Salum Said,
Rajabu Mpita na Haji Sheluhenda, Abdul Ahmed, Bakari Mwambele, Ramadhani
Fadhili na Awadh Juma.
Wengine ni Omari Mkwau, Kassim Chobo,
Abubakari Bakari, Ramadhani Milambo, Hamis Ndeka, Athuman Juma, Abdallah Salum,
Juma Makoti, Bashir Kakatu, Imam Omari, Rashid Lukuta, Bakari Athumani, Mbwana
Kassim, Nurdin Ahmed, Mustapha Mide, Rajabu Kifumbo, Zuberi Juma.
Wengine ni Omari Mkandi, Idrisa
Katulimo, Sawali Mola, Said Dudu, Ramadhani Juma, Mussa Sinde, Issa Sobo,
Yahaya Salum, Jabil Twahil, Shomari Tarimo, Hashim Bendera, Waziri Toy, Athuman
Yahaya, Yasin Seleman, Shaban Malenda, Yasin Mohamed, Khatib Abdallah na Rajabu
Rashid wote wakazi wa jijini Dar es Salaam.
Awali, ilidaiwa kuwa katika siku ya
tukio, wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja
walikula njama za kufanya maandamano isivyo halali.
Shtaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na
eneo la tukio la kwanza, washtakiwa walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo
la kusababisha uvunjifu wa amani.
Shtaka la tatu ilidaiwa kuwa washtakiwa
wote kwa pamoja walikiuka amri ya Jeshi la Polisi ya kutoa zuio la kufanya
maandamano na kufanya mkusanyiko ulisababisha vurugu na uvunjifu wa amani.
Katika shtaka la nne, ilidaiwa kuwa mshtakiwa
Makame, Idd na Nandumbi, waliwashawishi wananchi kwa kuwasambazia vipeperushi
vya kuhamasisha kufanya maandamano yasiyo halali.
No comments:
Post a Comment