Na Theonestina Juma, Kagera
DIWANI wa
Ka t a y a Ch o n y o n y o (CCM) wilayani Karagwe, Arnold Rweshekerwa,
amenusurika kuuawa na kundi la majambazi waliomteka nyara katika eneo la
Kyanyamisa kabla ya kuwatoroka akiwa amewafungia ndani ya gari lake katika Pori
la Kimisi
.Tukio hilo
limetokea siku chache tangu Rais Jakaya Kikwete, atoe siku 14 kwa majambazi
katika mikoa ya Kagera, Geita na Kigoma kusalimisha silaha na kuacha vitendo
hivyo kabla ya msako wa nyumba kwa nyumba kuanza.
Pia agizo hilo
la Rais Kikwete liliwahusu wahamiaji haramu waliopo katika mikoa hiyo kuwa
wameondoka ndani ya kipindi hicho.
Kwa mu j i b u wa h a b a r i zilizopatikana mjini
hapa na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Phillip Kalangi,
tukio hilo lilitokea Agosti 10, mwaka huu saa 2.00 katika eneo lenye kibao
kinachoonesha sehemu ya hifadhi ya akiba katika pori la Kimisi kuelekea
wilayani Ngara.
Baada ya kunusurika kuuawa na majambazi hayo,
waliteketeza gari la diwani huyo kwa kitu kinachodhaniwa bomu. Habari hizo
zinaeleza kuwa, Diwani huyo alikuwa ameenda Kijiji cha Kyanyamisa kumtembelea
bibi yake mzaa mama, ambapo wakati akirudi nyumbani alikutana na watu wawili
njiani, wakiwa na bastola, ambapo baada ya kumsimamisha walimtaka ageuze gari
kurudi alikokuwa anatoka.
Wakati wa harakati za kugeuza gari hilo,
huku majambazi hao wakiwa wamekaa ndani ya gari lake hilo
alikutana na watu wengine tena.
Alisema watu hao walikuwa na mifuko minne iliyojaa
bunduki, magazine na risasi, ambapo akiwa anawaendesha kwenye gari lake, watu
hao walikuwa wanaingiza risasi kweye magazine.
Walipofika mbali jirani na hifadhi ya akiba
walimwamuru diwani huyo kusimamisha gari na kuzima taa, huku wakiendelea
kuingiza risasi kwenye magazine kwa tochi.
Wakiwa katikati ya Pori la Kimisi alifunga milango ya gari kisha
kuruka kwa kupitia dirishani kutokomea porini.
Habari hizo zinaeleza kuwa diwani huyo alitembea
zaidi ya kilomita mbili akirudi Karagwe, ambapo aliona pikipiki moja ikiwa na
watu wawili wenye silaha wakitokea Kyanyamisa kwenda Ngara.
I n a d a i w a a l i s h i n d w a kuwasimamisha
kwa kuhofia huenda wakawa ni wenzao, wakati alipokuwa ametekwa aliwasikia
wakiwasiliana na watu wengine.
Baadaye alipata usafiri wa Hiace iliyokuwa ikitoka
Benako wilayani Ngara saa 3.30. Alipanda gari hilo ambapo alianza kuwasimulia abiria
kilichotokea. Habari zaidi zilieleza kuwa abiria hao walimwambia kuwa waliona
gari likiteketea kwa moto.
Kamanda Kalangi alisema; “Tu k i o h i l o l i p o n
a g a r i limeteketezwa kweli, lakini suala la utekaji wa diwani huyo, inakuwa
ngumu kulithibitisha kwani wakati likitokea, alikuwa peke yake.”
Ka t i k a t u k i o , wa t u h a o hawakuweza
kumdhuru diwani huyo, bali walimpora simu, sh.100,000 na viatu vyake alivyokuwa
amevaa.
Diwani huyo amelazwa Hospitali Teule ya Nyakahanga
baada ya kupoteza fahamu.
No comments:
Post a Comment