Na Mosi Mrisho
HATUA ya kwanza
ya usajili wa wachezaji kwa msimu wa 2013/2014 imefungwa rasmi juzi, ambapo
klabu zote za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zimewasilisha usajili wa vikosi vyao
ndani ya wakati.Akizungumza Dar es Salaam jana Ofisa
Habari wa Shirikisho la Mpira wa Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface
Wambura alisema baadhi ya klabu zimefanya makosa madogo madogo katika usajili
ambapo zilipewa jana kufanyia marekebisho kasoro hizo
.Alisema leo majina ya vikosi vyote
yatabandikwa kwenye mbao za matangazo za TFF kwa ajili ya kipindi cha pingamizi
kitakachomalizika Agosti 12 mwaka huu.Ofisa huyo alisema Kamati ya Sheria na Hadhi
za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake, Alex Mgongolwa itakutana Agosti 13 na 14
mwaka huu kupitia na kufanyia uamuzi usajili wa wachezaji wenye matatizo.
"Hatua ya pili ya usajili itaanza
tena Agosti 14, mwaka huu ikihusisha wachezaji ambao watakuwa hawajasajiliwa
katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu na wale kutoka nje ya Tanzania."Hivyo, dirisha la uhamisho kwa wachezaji wa
kimataifa litafungwa baada ya hatua ya pili ya usajili kumalizika Agosti 29,
mwaka huu," alisema Wambura.
No comments:
Post a Comment