07 August 2013

MBUYI TWITE ARUDI RASMI YANGA


 Na Mwandishi Wetu
BEKI wa Yanga, Mbuyi Twite ameanza mazoezi baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda kutokana na kupata kidonda katika paja.Mchezaji huyo ambaye aliumia wakati akiitumikia timu hiyo, alilazimika kupatiwa daktari bingwa kwa ajili ya kumpatia matibabu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, beki huyo raia wa Kidemokrasi ya Congo (DRC), alisema kwa sasa amepona na ataanza mazoezi na wenzake kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu inayotarajia kuanza Agosti 24, mwaka huu.
"Kwa sasa nipo fiti namshukuru Dokta wangu kwa kuweza kuwa karibu na mimi muda wote nilipokuwa na maumivu hadi kupona na kujiunga na wezangu," alisema Twite.
Alisema baada ya kupoana na atafanya mazoezi ya nguvu, kwa kuwa msimu unaokuja anataka kufanya makubwa uwanjani, ili kuitendea haki Yanga

No comments:

Post a Comment