07 August 2013

KIBOKO WA SIMBA,YANGA ATUA COASTAL UNION


Na Nasra Kitana
KLABU ya Coastal Union imefanikiwa kuipata saini ya kifaa cha timu ya Mamlaka ya Mapato ya Uganda (URA), Yayo Kato ambaye alizisumbua Simba na Yanga katika mechi za kirafiki zilizopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Timu hiyo ilipata nafasi ya kucheza na URA katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga katika mechi kali na kuifunga bao 1-0
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Khasim El Siagi alisema wamemsajili mshabmbnuliaji huyo baada ya kuvutiwa na uchezaji wake wakati timu yake ya URA ilipokuja kucheza nchini.Alisema kusajiliwa kwa mchezaji huyo kunaifanya timu yake kuwa na wachezaji wawili wa kigeni akiwemo raia wa Kenya Jerry Santo, ambaye yupo tangu msimu uliopita.
"Tulivutiwa na mchezaji huyo baada ya kumuona alivyocheza vizuri katika mechi za Simba na Yanga, na kuona anatufaa na kuanza kumfuatili ili kupata saini yake," alisema.giAlisema msimu huu wameamu kujipanga kiushindani na ndiyo maana wamefanya usajili wa umakini, lengo likiwa kupata nafasi za kuiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa.
Siagi alisema usajili wa mchezaji huyo, ndiyo wa mwisho na wana uhakika atakuwa msaada mkubwa kwao akishirikiana na wachezaji aliowakuta.Licha ya mchezaji huyo raia wa Uganda, Coastal Union pia imesajili wachezaji nyota Uhuru Selemani, Haruna Moshi 'Boban' na beki Juma Nyoso waliotokea Simba

No comments:

Post a Comment