- WAPO WATANZANIA,RAIA WA MATAIFA MENGINE
Na
Mwandishi Wetu
WAKATI Serikali ikiendelea k u u s a k a
m t a n d a o unaofanya biashara ya dawa za kulevya nchini, Jeshi la Polisi
Kitengo cha Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya nchini, limekiri kuwanasa zaidi
ya watu 100 waliokuwa na dawa za kulevya na kesi zao zinaendelea mahakamani.
Akizungumza
na gazeti hili jana kwa njia ya simu, akitokea mkoani Dodoma,
Mkuu wa kitengo hicho, Kamishna Msaidizi (ACP), Godfrey Nzowa, alisema kati ya
watu hao, baadhi yao
kesi zao zipo Mahakama Kuu.
A
l i s ema k w a k a w a i d a watuhumiwa wanapokamatwa na dawa hizo,
hufunguliwa mbele ya mashahidi akiwepo mtuhumiwa mwenyewe ili kuthibitisha na
baadaye kupelekwa mahakamani kama kielelezo na mahakama hupata fursa ya
kuzifungua na kuziangalia kama ndizo zenyewe.
"Wakati
kesi ikiendelea, dawa hizo huhifadhiwa ambapo kesi ikimalizika na kutolewa
hukumu, ma h a k ama h u t o a amr i y a kuteketezwa ambapo mwaka 2012,
Mahakama Kuu iliteketeza kilo 92.
Kamishna
Nzowa alikwenda mbali zaidi na kuweka wazi takwimu za watuhumiwa waliokamatwa
na dawa hizo kuanzia mwaka 2009 hadi Mei mwaka huu na kudai kuwa, hadi sasa
zaidi ya kilo 841.3 za cocaine, 175.64 za heroine na 10.8 (bangi), zimekamatwa.
Orodha
ya majina ya watuhumiwa na dawa walizokamatwa nazo kwenye mabano ni pamoja na
Steven Gwaza, (heroin gramu 825.7), Rebecca Wairimu Mwangi (heroine gram
1,800), Khatibu Bakari Khatibu na Khalid Salim Maunga (cocaine gramu 1,007.4).
Wengine
Dhoulkefly Awadh (cocaine gramu 893.58), Abdallah Pashua Kipevu (heroine gramu
31,000), Diaka Brama Kaba (heroin gramu 31,000), ambaye alikamatwa akiwa na
wenzake Ndjane Abubakar, Sylivia Kaaya Namirembe, Farid Kisuule, Robinson Dumba
Teise na Ismail Mugabi.
Wengine
ni Rashid Salim Mohamed, (cocaine gramu 1,374.32), Mini Thabo Hamza (cocaine
gramu 1,595.74), Hamis Mohamed Mtou (cocaine gramu 850), Kwako Sarfo, Mnigeria
(cocaine gramu 1,1951.80), Mustapha Musa (cocaine gramu 286), aliyekuwa na Aman
Saidfadhil Daruweshi na Afshin Jalal.
Jack Vuyo, (heroine gramu 42,000) huyu alikuwa na Anastazia Elizabeth Cloete, Simon
Eugenio Fadu(cocaine gramu 8,000), Assad Aziz, (heroine gramu 50,000), alikuwa
na Isamil Shebe Ismail, Rashid Salim na Majed Gholamghader.
Anna Jamaniste
Mboya, (cocaine gramu 1,140), Fredy William Chonde (heroine gramu 175,000),
Kambi Zuber, Abdul Ghan na Shahbaz Malik, Livinus Malik (Wapakistani)
waliokamatwa na (cocaine gramu 804.7).Chukwudu Denis
Okechukwu, Paulo Ekechukwu na Hycenth Stan (Wanigeria) (cocaine gramu
81,000).Shoaib S.O. Mohammed, Fedro Alfredo Chongo, (cocaine gramu 1,530).
Kadiria Said
Kimaro (heroine gramu 1,365.91), Abdallah Rajab Mwalimu (cocaine gramu 716.5),
Mwiteka Godfrey Mwandemele (cocaine gramu 1,112), Abbas Kondo Gede (cocaine
gramu 1,112), Mwanaidi Ramadhan Mfundo (cocaine gramu 5,000), ambaye alikuwa na
Sarah David Munuo.
Antony Karanja,
Benny Ngare, Almasi Hamis Said, Yahya Haroun Ibrahim, Aisha Said Kungwi, Rajab
Juma Mzome na John William Mwakalasya, Ally Mirzai Pirbakhshi (cocaine gramu
97,000) alikuwa na Aziz Juma Kizingiti, Said Mashaka Mrisho, Abdulahman Mtumwa
na Hamidu Kitwana Karimu.
Ramadhan
Athuman (heroine gramu 3,000) alikuwa na Rashid Mohammed, Ally Mohammed Kichaa
na Issa Abdulrahman.
Rashid Ally
Mtopea (heroin gramu 12,000) alikuwa na Idd Adam Mwaduga, Nurdin Adam, Maurine
Amatus Lyumba, John Adams Igwenma wa (Mnaijeria) ( cocaine gramu 830.19). Upendo Mohammed Cheusi, Abdallah Omar
Salum (cannabis sativa gramu 1,000) alikuwa na Cosmos Chukwumezie, Ifeanyi
Malven Kalu Oko (Wanaijeria) (heroin gramu 3,185.38), Allan Duller (cocaine
gramu 3,882.92), Alberto Mendes kutoka Ghana, (gramu 1,277.10 za heroine)
Wengine ni Joseph Chukwumeka
Nwabunwanne ambaye ni raia wa Nigeria, (gramu 1,245.96 za heroin) Kwaku Safo
Brobbey Mghana (gramu 13,781.78 za heroine), Princewill Ejike Mnigeria (gramu
981.12 za heroin), Mary Mvula Mzambia (gramu 391.51 za cocaine), Waziri Shaban
Mizongi, (gramu 2,013 za heroine) akiwa na Santos Joseph Mpondela, Kelvin
Kelven Mwazeni.
Wengine ni Emmanuela Adam, Mghana
(gramu 9,838.1 za cocaine), Asha Omary Ramadhan, (gramu 1.56), Mariam Mohammed
Said, (gramu 9,857.54 za bangi) akiwa na Abdullatif A. Fundikira.Aliendelea kuwataja Marceline Koivogui,
Mghana (gramu 1,073.82 za heroin), Edwin Cheleh Swen Mliberia (gramu 1,509.35
za heroin), akiwa na Benjamin Obioma Onuorah wa Nigeria, Sofia Seif Kingazi, (gramu
3,379.54 za cocaine) na Josephine Mumbi Waithera Mkenya (gramu 3,249.82 za
cocaine).
Iddi Juma Mfaume,(gramu 563.25 za
heroine), Amina Kassim Ramadhani,(gramu 1,980.11 za heroine) na Vivian Edigin
Mnigeria (gramu 797.56 za cocaine), Hadija Tambwe, (gramu 33,507.04 Za
cannabis), Sasha Farhan na Mnyeke Sativa, na Mychel Andriand Takahindangeng
Muindonesia, gramu 3,932.44 za cocaine).
We n g i n e n i K r i s t i n a
Biskavevskaja Mluthenia (gramu 4,000 za cocaine), Stephen Basil Ojiofor Mnigeri
(gramu 1,173 za cocaine), Judith Marko Kusekwa, (gramu 1,793 za heroine),
Khamis Said Bakari (gramu 1,793 za heroine).Kundi la mwisho ni Tabia Omary au Neema
Omary (gramu 994.97 za heroine), Masesa au Habiba Andrew Joseph, (gramu 1,037.9
za heroin). Hivi karibuni Agness Gerald "Masogange" na mwenzake
walikamatwa Afrika Kusini wakiwa na kilo 150 za dawa hizo.
Akizungumzia sakata la Mtanzania
anayedaiwa kukamatwa Mjini Dubai, Falma za Kiarabu, juzi akiwa na kilo tatu ya
dawa za kulevya aina ya cocaine, alisema yupo safarini hivyo suala hilo atalitolea ufafanuzi
leo baada ya kufika ofisini.
Dawa hizo zinadaiwa kuwa na thamani ya
Diraham milioni tatu, (sawa na sh. bilioni 1,321.7 za Kitanzania).Kwa mujibu wa mtandao wa Yahoo News, ambao haujataja jina la
mwanamke huyo, ulisema dawa hizo ziliwekwa kwenye mabegi na baada ya kuhojiwa
na Maofisa Usalama wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Mjini Dubai, alidai kuwekewa
dawa hizo na rafiki wa mumewe nchini Brazil (hakutajwa jina).
"Mume wangu kupitia rafiki yake,
aliamua kunitumia kama punda niweze kuyabeba mabegi haya kwa kuyarudisha
nyumbani Tanzania,"
alisema mwanamke huyo wakati akihojiwa na Ofisa mmoja wa Polisi Mjini Dubai.
Kwa mujibu wa mtandao huo, mwanamke
huyo alikamatwa juzi akiwa katika harakati za kurejea Tanzania wakati akitoka mapumziko nchini Brazil ambapo
mumewe alimpa nafasi ya kwenda likizo ya miezi mitatu ili akapumzike."Wa k a t i n i k iwa k a t i k a
mapumziko nchini Brazil,
rafiki wa mumewe alinipa haya mabegi niweze kurejea nayo Tanzania,"
alidai mwanamke huyo wakati akihojiwa na kuongeza kuwa;
"Mume wangu amenisababishia
matatizo kwa kunipa nafasi ya kupumzika miezi mitatu nchini Brazil,"
aliongeza.Hata hivyo, mtandao huo ulidai mtuhumiwa huyo amepelekwa
katika Mahakama ya Umma ili taratibu za kisheria ziweze kuchukua mkondo wake.
Watakao kamatwa siku zote ni wale wanaotumiwa. Wanaowatuma, ambao ni mafisadi papa hata siku moja hawatakamatwa maana wanajuana na mtandao wa maofisa hao wa vyombo vya dola wanaofanya nao hizo dili.
ReplyDeletehawa watu pichazo zingewekwa pia, ingekuwa poa sana kwani unaweza kuta hapa anajina hilo lakini kitaa anatumia jingine pia hata watu wangeweza saidia huenda anawatu wa karibu nao wangechunguzwa pia.
ReplyDeleteNa hayo majina ni ya mwaka huu tu au toka enzi ya nyerere yakawa bado yanafanyiwa kazi
Acheni kuwaumiza njaa kali wakati wenye biashara hizo wapo wametuli wakisema. "jamani tule pozi kidogo hali sio shwari sana kisha tutaendelea"
Deletehakuna kitu hapo . hayo majina feki wameweka tu ili serikali isifikirie mbali , ikea kupanga mikakati juu ya hii orodha feki.
ReplyDeleteWatanzania wa lei si wa jana . hatudanganyiiiiiiki
JE KULE MEXCO ,VENEZUELA NA AFRIGHANSTAN WANAFANYA NI DAGAA TANZANIA KILA MTU NI POLISI,HAKIMU NA JESHILA MAGEREZA
ReplyDelete