28 August 2013

MADIWANI BUKOBA SASA KICHEKONa Mwandishi Wetu, Dodoma
KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CCM), imetoa maamuzi juu ya sakata la madiwani wanane waliotangazwa kufukuzwa uanachama na Halmashauri kuu ya chama hicho mkoani Kagera hivi karibuni.
Katika maamuzi yake, Kamati Ku u ime b a t i l i s h a u amu z i uliofanywa na Halmashauri Kuu CCM, mkoani humo Agosti 13 mwaka huu wa kuwafukuza uanachama madiwani haoKutokana na maamuzi hayo, madiwani hao ni wanachama halali wa chama hicho.Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nnauye, ilisema Kamati Kuu imetoa uamuzi huo baada ya kubaini kuwa, Halmashauri Kuu ya CCM, mkoani humo haikuzingatia katiba ya chama ya 1977,toleo la 2012 Ibara ya 93 (15).
Ibara hiyo inasomeka kuwa moja ya kazi ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa ni kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho unafanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa, isipokuwa suala la kumvua uanachama au uongozi diwani, lisifanyike hadi Kamati Kuu imearifiwa na kutoa maelekezo.
Kamati Kuu imewaonya madiwani wa CCM Manispaa ya Bukoba, Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki na Meya wa Manispaa ya Bukoma Mjini, Dkt. Anatory Amani kwa kusababisha kukosekana utulivu, mshikamano na amani katika manispaa na ndani ya chama.
Pia kamati hiyo imeitaka Serikali kumwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi maalumu juu ya mambo yanayolalamikiwa dhidi ya Dkt. Amani ili ukweli uweze kujulikana na matokeo ya uchunguzi huo yawasilishwe kwenye Baraza la Madiwani ili hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria na taratibu zinazoongoza Serikali za Mitaa.
Wakati tuhuma hizo dhidi ya Meya zikichunguzwa, Kamati Kuu imewataka madiwani hao kurejesha utulivu kwenye manispaa na chama ili kufanikisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuwaletea maendeleo wananchi wa Bukoba. fukuzwa uanachama na Halmashauri Kuu ya chama hicho, mkoani Kagera, hivi karibun

3 comments:

 1. Kesi, mnajaribu kuimaliza kishwahiba!

  Mnachofia ni kupoteza jimbo wakati wananchi wa chini ndio wanaoumia sana. Hebu fikiri tangu mgogoro uanze karibu sh. 100milioni za mapato yanayotokana na ushuru wa soko zimepotea, halafu mnacheka na Kagasheki as if anachofanya na madiwani hao ni kizuri!

  Huu ni uharo! mnaonesha jinsi gani mko dhaifu na ijulikane wazi kuwa hata mngeziba viraka namna gani hii nchi itapata mabadiliko ya kisiasa tu. Sasa msitumie nguvu nyingi ambayo inaendelea kudhoofisha watu.

  ReplyDelete
 2. hawa wapuuzi kweli...wananchi tumechoka kufanywa wajinga.

  ReplyDelete
 3. Mimi nafikiri wananchi wa Bukoba siyo wajinga kiasi hicho tunavyofikiri, wanajua chanzo cha mgogoro na athari zake. Hivi kujenga soko jipya ni dhambi? hivi kuwa na viwanja vyenye hati milki ni dhambi? Kumbe mabadiliko yanawezekana siyo lazima kuwa na fedha za kuhonga. Big up Amani na maendeleo!

  ReplyDelete