Trafiki feki akiwa amesimama akiwa amevalia sare za trafiki huku ameshikilia jadala lake la kazi.
- ANA CHEO CHA SAJINI,VITABU VYA KOTOZA FAINI
- WANANCHI WATOA USHUHUDA JINSI WANAVYOMFAHAMU
Na
Waandishi Wetu
MSEMO wa mjini mipango, umejidhihirisha wazi baada ya
Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam
kumkamata askari bandia wa kikosi cha usalama barabarani akiwa amevalia sare za
trafiki akiendelea na kazi pasipo kugundulika kwa siku kadhaa kuwa anafanya
uhalifu.
Trafiki
huyo bandia mwenye cheo cha
sajini, (jina halikupatikana) alikamatwa na Polisi akiwa 'kazini' maeneo ya
Tabata Kinyerezi akiwa amevaa sare mpya ya Askari wa Usalama Barabarani, kikoti
cha kuakisi mwanga na kofia nyeupe.
Pia trafiki huyo alikuwa na
jalada pamoja na kitabu cha kutoza faini (Notification) kwa madereva
wanaopatikana na makosa ya kukiuka sheria za usalama barabarani.
Gazeti hili lilishuhudia
trafiki huyo feki akiwa amekamatwa na Polisi na kisha kufikishwa Kituo Kikuu
cha Polisi Kati, huku akijifanya amepoteza fahamu.
Mashuhuda waliozungumza na gazeti hili, walisema
wanamfahamu trafiki huyo kwa muda mrefu kiasi kwamba madereva wengi
wanamuogopa, kwani akikamata gari hakuna cha majadiliano kama
ilivyo kwa wengine, bali anawatoza faini moja kwa moja kati ya sh. 20,000 hadi
25,000.
"Yule tunamfahamu kwa uchapaji kazi, alikuwa
hataki rushwa hata kidogo, akikukamata ujue umeumia, lazima akuandikie
'notification'," alisema dereva mmoja anayemfahamu trafiki huyo kwa muda
mrefu.
"Wakati wa foleni alikuwa akisimama barabarani
na kuanza kuyaongoza magari, lakini alipoona imekuwa kubwa zaidi alikuwa
akiondoka kwa kuhofia kujulikana," alisema shuhuda mwingine.
Mkazi mmoja wa jijini Dar es
Salaam anayemfahamu trafiki huyo, alisema; "Namfahamu huyu
jamaa mambo yake ni mazuri sana
nyumbani kwake, hivi sio trafiki... ahaaa haiwezekani bwana."
Aliongeza kuwa; "Yule trafiki huwa anatanua sana kwenye baa na kama
kulikuwa na ugeni wa viongozi hasa wa nje alikuwa akisema anawahi kwenda
kulala, kwani ataamka mapema kwenda kuongoza misafara."
B a a d h i y a m a d e r e v a wanaomfahamu
trafiki huyo, walisema hawaamini kama kweli
mtu huyo ni trafiki feki kwani wakati mwingine alipokutana na askari wenye vyeo
vidogo chini yake walimsalimia kijeshi.
Mashuhuda hao walisema trafiki huyo alikuwa
akifanyakazi kwenye maeneo ya Mkuranga na wakati mwingine alionekana
akiwapangia kazi vijana walio kwenye vikundi vya Polisi Jamii ambao wanasaidia
kuongoza magari. Kwa mujibu wa watoa taarifa hao, vijana wa Polisi Jamii
walipomkamata dereva amekiuka sheria za barabarani, walielekezwa kwa trafiki
huyo ambaye bila mjadala aliwaandikia notification.
Watu waliotoa maoni kuhusu tukio hilo, walilihusisha na uzembe katika Jeshi la
Polisi kiasi cha kushindwa kujitambua. "Hawa wenzetu Jeshi la Polisi
hawajajitambua, haiwezekani watu washindwe kutambuana wakati wanafanyakazi
pamoja na mtu huyo," alisema John Edward.
Lakini pamoja na kulishutumu Jeshi la Polisi,
baadhi ya watu walionekana kufurahishwa na kitendo cha trafiki huyo feki
wakisema ni mbunifu wa ajira.
"Ingawa
amefanya makosa kwangu mimi naona ni mbunifu wa ajira na amelisaidia sana jeshi la Polisi kwani walikuwa wanakaribia eneo lake
la kazi madereva walikuwa waangalifu sana
ili kuepuka kupigwa notification," alisema Edward.
Kweli majanga... Wanamziki wamtungie nyimbo tu trafiki feki wetu wa bongo...awe maarufu ..ameutafuta umaarufu kwa bidii yote mwacheni awe maarufu aifaidi nchi.
ReplyDeleteJamaa ni kiboko kwa ubunifu 100% kwanza asitahili kupewa adhabu kali kwa vile amelisaidia jeshi la polisi kwa muda mrefu na kazi yake ilikuwa ya uhakika kuliko hata hao walioajiriwa Big up kamanda feki na m\Mungu atakusaidia katika majaribu hayo. Ila mazoea mabaya kwa wakati mwingine kama ni mtaji ulikuwa unatafuta si tayari ulikuwa umeshapata kwa nini usingebuni ajira nyngine bhana mdogo? ANYWAY MAJARIBU NI MTAJI
ReplyDeleteHuyu kweli ni mbunifu. Apelekwe CCP mara moja then awe polisi. Big up mkubwa
ReplyDeleteHuyu si mpumbavuwala simbunifu il yuko nyuma ya wakubwa huko juu , ww jiulize hizo nguo kapata wapi na hicho kitabu kaokota au kapewa, HiiniNchi ya Wadanganyifu Bwana mwacheni ale na WAKUBWAAAAAA.
ReplyDeleteMie nampongeza trafiki feki huyo aliyefanya kazi nzuri kupita wale walioajiriwa kihalali na wanaishia kubambikizia watu kesi za uwongo! Yupi afadhali? Ni afadhali huyu kuliko baadhi ya matrafiki wa kituo cha MAJENGO - Mjini Moshi!!! Sisi watu wa Moshi twavumilia mengi tungeomba tuletewe huyu trafik feki atusaidie!
ReplyDeleteAjira zimekuwa ngumu....Hongera kwa ubunifu baba!
ReplyDeleteNampa hongera sana
ReplyDeletedah hata mimi namkubali wala nsiyo huyo tu wapo wengi kimsingi jeshi la polisi linabidi kujipanga upya hii ni aibu ya mwaka
ReplyDeleteTusimlaumu ajira zimekuwa ngumu.
ReplyDeleteHeko wewe trafiki feki kwani ufeki wako haupo kwani umelisaidia taifa kuokoa pale ambapo ajali ingelitokea japokuwa hukuwa kwenye ajira
ReplyDeleteserikali itambua kuwa uhaba wa ajira ndio unapelekea mambo kama haya.
ReplyDeleteMimi nadhani tutafute kiini cha haya matatizo ya watu kujifanya Askali polisi . Askali polisi wachache wanaolitia doa jeshi zima ndo moja wapo za sababu zinazowafanya watu kujifanya Polisi. Kama mapolisi wangekuwa waaminifu , kusingekuwa na watu ambao wangejifanya polisi. Udhaifu wa baadhi ya Polisi ni mojawapo cha chanzo cha watu kufanya hivyo. maelezo tuyoyapata ni kwambo huyu bwana alikuwa anapiga faini kila kukicha na kitabu bandia. Vitabu hivyo hivyo bandia vimekuwa vikilalamikiwa na madereza kuwa fedha za makusanyo hayafiki serikalini. Kama ingekuwa kila anayekamatwa anapelekwa mahakamani huyo polisi feki asingebuni hiyo ajira. Mimi naomba Jeshi la polisi lijitazame, lijipime na pale lilipoteleza lijirekebishe kwa dhati kwa manufaa ya nchi. Sisi raia tutajuaje kama huyu trafikifeki au polisi wa doria feki tunaishia kulilaumu jeshi zima la Polisi. Kosa la kwanza si kosa bali kurudia kosa. Hivi nauliza mkuu wa kituo huwa hatembelei vituo ambavyo wamepangwa askali ao ni mkuu wa ofisi kwa kukaa oficini kwenye hewa baridi. Kama wangekuwa wanatembelea sehemu walizopangwa askari wao vitu kama hivyo visingetokea. Narudia, tujiangalie, tujipime na tujirekebishe pale tulipokosea
ReplyDelete