Mosi Mrisho na Namkeshe Ridhiwani
MWA K I L I S H I w a Ta n z a n i a k a
t i k a mashindano ya Big Brother Africa 'The Cheser', Feza Kessy amewashukuru
Watanzania kwa kumpigia kura na kumwezesha kubaki katika jumba la Big Brother
Afrika Kusini kwa wiki 11.
Akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Feza
alisema katika shindano hilo
amejifunza mambo mengi na pia alikutana na changamoto ambazo alikabiliana nazo.
F e z a a l i s
ema mo j a y a changamoto alizokutana nazo ni tofauti ya tabia ambapo kila
mmoja alikuwa huru, kufanya anachotaka hivyo ilitokea kukwaruzana mara chache
akiwa katika jumba hilo.
Alisema
alijifunza uvumilivu alipokuwa Big Brother, kutokana na mambo mbalimbali
yaliyojitokeza ikiwemo la kusalitiwa na rafiki yake ambaye alikuwa mshiriki
kutoka Ghana.
"Nilijisikia vibaya kurudi
nyumbani bila ushindi, ila nimekubali matokeo na naamini niliiwakilisha vizuri
Tanzania na utanzania wangu uliniwezesha kuishi na watu wenye tabia
mbalimbali," alisema.
Naye Meneja Uhusiano wa Kampuni ya
Multi Choice Tanzania, Barbara Kambogi alisema anamshukuru, Feza kwa
kuiwakilisha nchi vizuri katika mashindano hayo mpaka Jumapili iliyopita ambapo
alitolewa.
Meneja huyo alisema, Feza alikuwa kati
ya washiriki bora waliokuwepo katika jumba la Big Brother, lakini anaamini
ataendelea kufanya vyema, baada ya kutoka na anamtakia kila la kheri katika
kazi zake za muziki.
Katika mashindano hayo ambayo huu ni msimu wake wa nane, Tanzania
iliwakilishwa na wawakilishi wawili, Feza na Ammy Nando ambapo mshindi
ataondoka na dola 300,000 za Marekani
No comments:
Post a Comment