Rehema Maigala na Darlin Said
KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
Tanzania, Ponda Issa Ponda, amesomewa mashtaka yanayomkabili chini ya ulinzi
mkali wa Polisi wodini katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI).Ponda alisomewa
mashtaka yanayomkabili jana jioni mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Hellen Liwa na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Tumaini Kweka
.Ilidaiwa na
upande wa mashtaka kuwa mshtakiwa huyo, Shekhe Ponda, anakabiliwa na mashtaka
mawili aliyotenda Juni 2 na Agosti 11, mwaka huu sehemu mbalimbali.Ilidaiwa kuwa
Shekhe Ponda alichochea vurugu sehemu mbalimbali za Tanzania. Ilidaiwa kuwa
Shekhe Ponda, Agosti 11, mwaka huu alihamasisha vurugu. Pia inadaiwa kuwa Juni
2, mwaka huu Ponda alishiriki tena kuhamasisha vurugu.
Sehekhe Ponda alikana mashtaka hayo na
kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 28, mwaka huu, ambapo mshtakiwa ataendelea
kuwepo hospitali kwa ajili ya matibabu.Akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya kusomwa kwa mashtaka hayo, Wakili wa Shekhe Ponda, Juma Nassoro,
alisema hati hiyo ina makosa kwani Agosti 11, mwaka huu siku ambayo anadaiwa
kutenda kosa hilo, alikuwa tayari amelazwa hospitalini, hivyo wataleta
pingamizi la kufuta kesi hiyo itakapotajwa.
Alisema leo walikubaliana a f a n y iwe
ma h o j i a n o kwa kumtuhumu kufanya uchochezi maeneo ya Zanzibar, Dar es
Salaam na Morogoro."Tulipinga yasifanyike mahojiano
hayo kwa kuwa Shekhe Ponda ameishawasilisha malalamiko yake Ofisi za Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora kutokana na polisi kudai kuwa hawajampiga
risasi Shekhe Ponda," alisema wakili huyo. Pia alisema Ponda ameishapeleka
malalamiko yake Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Aliongeza kwamba mahojiano hayo
hayakufanyika kutokana na hali ya Shekhe Ponda kutokuwa nzuri. "Lakini
baada ya saa tatu wamemsomea mashtaka kuanzia saa 10 jioni," alisema.Nje ya MOI ulinzi uliimarishwa na
hakuna mtu aliyeruhusiwa kuingia wodini kuangalia wagonjwa kwenye block
aliyolazwa Shekhe Ponda.
Magari ya Polisi yasiyopungua manne
yalikuwa yameegeshwa eneo hilo yakiwa na askari polisi waliojidhatiti kwa
silaha.Wafuasi wa Shekhe Ponda walisikika wakilalamika baada
ya kuzuiwa kuingia wodini kumuona na kuhoji; "Kila sehemu mnatuzuia,
tunahitaji kumuona Shekhe
No comments:
Post a Comment