20 August 2013

TOZO ZA LAINI,CUF YAMVAA MAKINDA CHAMA cha Wananchi (CUF), kimedai kusikitishwa na kauli ya Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda anayodaiwa kuitoa hivi karibuni, Mjini Bagamoyo, mkoani Pwani ili kushinikiza wananchi kulipa tozo ya laini za simu sh. 1,000 kila mwezi, anaripoti Mwandishi Wetu
.Naibu Mkurugenzi Habari, Uenezi na Haki za Binadamu wa CUF, Bw. Abdul Kambaya, aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.Alisema Bi. Makinda aliyasema hayo baada ya ufunguzi wa mafunzo ya wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC), Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Bajeti.
Aliongeza kuwa, katika ufunguzi huo Bi. Makinda alisema: “Haya maendeleo tunayotaka sisi kama Watanzania yatapatikana kwa kulipa kodi, hata vitabu vitakatifu vinasema kila mtu lazima achangie.”
Kutokana na kauli hiyo, Bw. Kambaya alisema chama hicho kinaamini kila vocha ya simu anayonunua mwananchi kuna asilimia zinazoingia katika mfuko wa Serikali.
“CUF tulitarajia kabla ya kufikiria jinsi ya kuendelea kumbebesha mzigo mwingine mwananchi, yeye kama msimamizi mkuu wa Bunge, wangeweka mikakati na mipango inayotekelezeka ya kumuinua mwananchi kiuchumi.

No comments:

Post a Comment