26 August 2013

SAKATA LA OFISA USALAMA:SIRI NZITO

  • ADAIWA KUTOA AMRI KWA VIGOGO WA POLISI
  • POLISI KUWEKA HADHARANI UTAPELI WAKE



 Na Mwandishi Wetu
SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kumnasa Bw. Alquine Masubo (42), akidaiwa kujifanya Ofisa Usalama wa Taifa, siri nzito juu ya vitendo vinavyodaiwa kufanywa na mtuhumiwa huyo, sasa zimeanza kufichuka.

Habari na picha zilizochapishwa na gazeti hili juu ya tukio la kukamatwa Bw. Masubo, ziliibua maswali mengi kwa baadhi ya wasomaji ambao baadhi yao walipiga simu katika chumba cha habari na kudai wao ni miongoni mwa waliotapeliwa na mtuhumiwa huyo.
Mkazi mmoja wa Dar es Salaam (jina tunalihifadhi), alisema mtuhumiwa ambaye huwa na kawaida ya kushirikiana na mke wa kigogo mmoja wa Jeshi la Polisi, amewahi kumbambikia kesi ya utapeli na kujitambulisha kwake kuwa yeye ni Ofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Alisema, baada ya kukamatwa na kufikishwa kituo kimoja cha polisi Dar es Salaam, mtuhumiwa alitoa agizo kwa Kamishna Msaidizi wa jeshi hilo (sasa ni mstaafu), atoe amri kwa RCO (Mkuu wa Upepelezi), aweze kukaguliwa nyumbani kwake
"Walipokwenda nyumbani kwangu na kukosa nyaraka ambazo walikuwa wakizitafuta, walichukua vitu mbalimbali ndani kwangu ambavyo ni pamoja na kitanda, godoro, sofa, kabati, friji, DVD, televisheni, redio kubwa na vingine vingi.
"Kabla hawajachukua vitu hivyo, alimwambia mdogo wangu ampe sh. milioni tatu ili nisichukuliwe vitu vyangu, alipewa sh. milioni moja, lakini bado alitoa amri vitu vyangu vibebwe licha ya kutoa risiti ya kila kitu walichochukua.
"Pia alimtaka mdogo wangu ampe pesa ili niweze kupewa dhamana mahakamani, kesi niliyobambikiwa dhamana yake ilikuwa wazi... aliwaambia waendesha mashtaka kuwa yeye ni Ofisa Usalama kutoka Ikulu, ambayo imemtuma ili nisipewe dhamana," alidai mkazi huyo.
Aliongeza kuwa, kutokana na agizo hilo alikaa gerezani miezi mitatu, lakini alisaidiwa kupewa dhamana kutokana na juhudi za dada yake ambaye ni karani wa mahakama (bila kumtaja jina wala mahakama anayoifanyia kazi jijini humo).
Mkazi huyo aliongeza kuwa, wakati akiwa mahabusu katika kituo kimoja cha polisi Dar es Salaam, mtuhumiwa (Masubo) alikwenda kituoni hapo na kumtaka atoe maelezo anayotaka yeye na asipofanya hivyo, atambambikia kesi kubwa zaidi.
"Nilikataa kuandika maelezo anayotaka yeye, wakati huo ndugu zangu walikuwa nje, mtuhumiwa aliwafuata na kuwaambia sitaki
 Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Dar es Salaam jana, Kamanda wa kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, alisema mbali ya tukio hilo, jeshi hilo pia litazungumzia mambo mengine makubwa waliyoyabaini.
"Mkutano wangu wa kesho (leo) na waandishi wa habari, nitazungumzia tukio hilo, pia kuna mambo mengine makubwa ambayo tunatarajia kuyazungumzia si hilo tu," alisema.
Aliongeza kuwa, tayari kuna kikosi maalumu cha polisi ambacho kinaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Mlipuko huo ulitokea juzi ambapo bomu hilo linadaiwa kutengenezwa kwa chupa na kujazwa petroli ambapo madhabahu, gari la mchungaji vinadaiwa kuungua.
Mchungaji wa usharika huo, Noah Kipungu juzi alisema chupa za bia zilizojazwa mafuta hayo zikiwa zimezibwa na mifuniko iliyotobolewa tundu, ziliwashwa moto ili kuchochea mlipuko huo.
Alisema katika tukio hilo, hakuna mtu aliyekufa wala kujeruhiwa zaidi ya watu kukumbwa na taharuki.
kutoa maelezo hivyo atanipoteza na sitaonekana tena uraiani.
"Nd u g u z a n g u wa l i k u j a kunibembeleza nibadilishe maelezo na kuandika aliyotaka mtuhumiwa, lakini nilikataa....baada ya kusoma habari za mtuhumiwa katika gazeti lenu (Majira), Ofisa mmoja wa polisi ambaye alihusika kumkamata Bw. Masubo, alinipigia simu na kunieleza usumbufu aliopata akitakiwa kumuachia mtuhumiwa.
Aliongeza kuwa, inawezekana mtuhumiwa amewatapeli watu wengi hivyo, Agosti 28, mwaka huu atakwenda Kituo cha Polisi Kati ili aweze kufikisha malalamiko yake.
"Kwa sasa nipo Tanga.. kwa shughuli zangu za kibiashara, narudi Dar es Salaam keshokutwa (kesho), Jumatano nakwenda kutoa malalamiko yangu dhidi ya huyo jamaa Kituo cha Polisi Kati," alidai.
Kamanda Kova
Kutokana na tuhuma hizo, gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, kama kuna baadhi ya watu waliojitokeza kulalamikia utapeli wowote waliofanyiwa na mtuhumiwa.
Katika majibu yake, Kamishna Ko v a a l i s ema j e s h i h i l o litazungumzia sakata la ofisa huyo leo saa saba mchana na kama kuna maswali yaulizwe katika mkutano huo.
"Wiki iliyopita nilizungumzia suala hili, katika kituo kimoja cha redio, lakini kama kuna maswali yoyote, mje kesho saa saba (leo) katika mkutano wangu na waandishi wa habari, nitazungumzia sakata zima la huyo Ofisa Usalama feki," alisema.
Akizungumzia juu ya mtuhumiwa kudaiwa kushirikiana na baadhi ya vigogo ndani ya jeshi hilo alisema; "Sifahamu lolote kuhusu hilo ila nalipokea, tutaanza kulifanyia kazi," alisema

1 comment:

  1. AJIRA NDIO TATIZO SASA WATU WANABUNI AJIRA.

    ReplyDelete