27 August 2013

TAMBWE,KAZE KUTAMBULISHWA KWA MASHABIKI SIMBA J'PILI



Na Elizabeth Mayemba
UONGOZI wa Klabu ya Simba unatarajia kuwatambulisha rasmi wachezaji wake wa kimataifa kutoka Burundi, katika mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Mafunzo ya Zanzibar itakayochezwa Jumapili ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wachezaji hao ni mshambuliaji Amisi Tambwe na beki Gilbert Kaze ambao tangu wasajiliwe na timu yao mpya ya Simba mashabiki wao hawakupata nafasi ya kuwashuhudia.Akizungumza Dar es Salaam jana Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala alisema, pamoja na wachezaji hao kuonekana kesho mjini Arusha wakati timu hiyo ikicheza na JKT Oljoro katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, mashabiki wa Dar es Salaam wao watawaona wachezaji hao Jumapili.
“Siku ya Simba Day wachezaji hawa hawakuonekana mbele ya mashabiki wetu, hivyo Jumapili tutatumia nafasi hiyo kuwatambulisha rasmi kwa mashabiki na wanachama wa Simba,” alisema Mtawala.Alisema kwa kuwa vibali vya kufanya kazi nchini vya wachezaji hao vimepatikana, hivyo ni nafasi nzuri kwa wana-Simba kuona burudani kutoka kwa wachezaji hao ambao walikuwa wakisubiriwa kwa hamu kubwa. 
  Mwenyekiti wa Simba Aden Rage alifanikiwa kupata Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) za wachezaji hao baada ya juzi kupanda ndege hadi Burundi kwa ajili ya kushughulikia suala hilo.Rage alisema alilazimika kuingilia kati suala hilo kwa sababu lilihusu baadhi ya taratibu muhimu za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na ukweli kwamba viongozi wa  Vital’O, klabu waliyotoka wachezaji hao hawakuwa mjini na hivyo kuchelewa kwao kungeigharimu Simba. S i m b a walianza L i g i Kuu kwa kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Rhino Rangers mechi i l i y o c h e zwa Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.

No comments:

Post a Comment