28 August 2013

PTA YAZIDI KUONGEZA UFANISINa Frank Monyo

MAMLAKA ya Bandari Ta n z a n i a ( T PA) , imeendelea kufanya maboresho katika utendaji kazi kwa upande wa Bandari ya Dar es Salaam ili kuongeza ufanisi wakati wa kuwahudumia wateja wake.Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana, Meneja Mawasilino wa TPA, Janeth Ruzangi, alisema juhudu za pamoja kati ya wadau na mamlaka zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuongeza ufanisi katika bandari hiyo.

"Mafanikio yaliyopatikana ni kuongezeka kwa shehena kutoka tani milioni 10.9 kwa mwaka 2011/12 hadi kufikia tani 12.5 mwaka 2012/13 ikiwa ni ongezeka la asilimia 15.0 pia katika shehena yote iliyohudumiwa mwaka 2012/13,shehena za chini zitumiazo bandari (landlocked countries) ilikuwa tani milioni 4 ambayo ni sawa na asilimia 32 ya shehena," alisema Ruzangi.

Alisema shehena yote ya mizigo ya nchi 6 zitumiazo Bandari ya Dar es Salaam; za Zambia, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Burundi, Rwanda na Uganda imeongezeka kutoka tani milioni 3.55 mwaka 2011/12 hadi kufikia tani milioni 4.05 mwaka 2012/13. Alisema ongezeko hili ni asilimia 14.2.

Aliongeza kuwa muda wa ukaaji wa meli bandarini umepungua kutoka siku 6 hadi siku 4 ambapo ni sawa na asilimia 19.7 wakati idadi ya siku kwa meli kusubiri nje kuingia ndani kwenye gati imepungua kutoka siku 3 hadi kufikia siku 1 mwaka 2012/13 kinyume na siku 28 zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

"Hata hivyo, kasi ya kupakua magari imeongezeka kutoka upakuaji wa magari 343 kwa shift hadi magari 672; ongezeko hili ni asilimia 95.9," alisema Ruzangi.

Alibainisha sababu za kuongezeka kwa ufanisi huo kuwa ni hatua zilizochukuliwa na serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi kwa kusimamia kwa karibu utendaji kazi wa mamlaka hiyo.

No comments:

Post a Comment