28 August 2013

DOLA MIL.100/- KUWEKEZWA MRADI DARTSNa Grace Ndossa
DOLA za Marekani milioni 100 zinatarajiwa kutumika kununua mabasi ya Mradi wa Mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam kwa upande wa sekta binafsi.Hayo yalibainishwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Mifumo na Uendeshaji wa DARTS, John Mashauri, wakati akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana.

Alisema sekta binafsi ndiyo itakuwa inahusika katika ukusanyaji wa nauli pamoja na utunzaji wa fedha katika mradi huo ili kudhibiti upotevu wa fedha.Alisema zabuni za ununuzi wa mabasi na uwekezaji kwenye mfumo wa ukusanyaji nauli na utunzaji wa fedha zinafanyiwa mapitio zilingane na uhalisia kitakwimu na uendeshaji kutokana na muda mwingi kupita tangu ziandaliwe.
"Utoaji wa huduma kwenye mfumo wa wakala wa usafiri wa haraka unahusisha zaidi sekta binafsi na unatarajiwa kuwekeza dola milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa mabasi na mfumo wa ukusanyaji wa nauli na utunzaji wa fedha ambazo zinatakiwa kuwa tayari mfumo unapoanza kufanya kazi," alisema Mashauri.
Alisema mradi wa DARTS umepata mshauri Mwelekezi Mkuu ambaye atasaidia wakala kufanikisha azma yake ya kukamilisha utekelezaji wa shughuli za ujenzi wa miundombinu na upatikanaji wa watoa huduma katika mfumo huo.
Mashauri alisema katika utekelezaji wa mradi huo awamu ya kwanza jumla ya daladala 1,600 zitahamishiwa sehemu nyingine kupisha mabasi yaendayo haraka katika jiji la Dar es Salaam.Alisema kwa sasa wanaandaa mkutano maalum wa wamiliki wote wa daladala ili kuendelea kuwahamasisha wajiunge katika kampuni na baadaye wanunue hisa.
Akizungumzia kuhusu fidia, alisema tayari wafanyabiashara 230 waliokuwa katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo wamelipwa na wakazi wa Magomeni Bondeni 42 wamelipwa na kupisha uhamisho wa nguzo za umeme.Kwa upande wa Kariakoo Gerezani, alisema wakazi 81 kati 106 wamekwishalipwa fidia zao na baadhi yao bado taratibu zinaendele

No comments:

Post a Comment