22 August 2013

PINDA ATAKA WATANZANIA KUTUMIA ATM



Na Mwandishi Wetu
WAZIRI M kuuMizengoPind a,ame wataka Wa tanzaniakua cha tabia yakutemb eanapesamkonon ib adalayake wa tumie mashinez akibenk i (ATM)katikakuhifadh i fedha zao kwa ajili ya usalamawao.Hayo aliyaba inisha j anaji jini Dar esSalamakatikahaf layauzind uz iwa hu dumaya Kadi mpyayaA TMyabenki yaC RDBijulika nayok ama‘TemboCardChinaUnio nPay’ ,itakayotu mika bainayanc hiyaChinan aTanzan iaili kuw e zaku rah isisha hu dumaza kibiashara katika nchi hizo.

Pinda alisema kuwa kwa kutumia mfumo wa kadi wa kibenki, utaweza kuzuia wezi kutumia nafasi ya kuiba au kupora fedha kwa watu hasa wafanyabiashara pindi wabebapo fedha za biashara mifukoni mwao."Naipongeza sana benki ya CRDB kwa kuzindua huduma hii ambayo itawapa fursa wafanyabiashara wa Tanzania na China kuweza kufanya biashara zao kwa umahiri na umakini na kuwafanya wafanyabiashara hao kuhifadhi fedha mahali pa usalama ambapo sehemu yoyote wahitajipo huduma ya fedha wanaweza kupata kwa urahisi," alisema Pinda.
Alisema kuwa asilimia kubwa ya Watanzania bado wanatabia ya kutembea na fedha mifukoni kwa lengo la kuonekana kuwa wana uwezo wa kumiliki fedha nyingi, hali hiyo ni mbaya kwani inawafanya wezi kupata nafasi ya kuiba kwa urahisi zaidi.Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Dkt.Charles Kimei alisema kuwa benki ya CRDB imeweza kupanua wigo wake katika kuwafikia wafanyabiashara wote wa nchi ya Tanzania na China, kwa kuwapa fursa ya kuhifadhi fedha zao katika benki hiyo ambayo itawapa urahisi zaidi wa kufanya shughuli zao za kibiashara wakati watakapohitaji huduma ya kifedha.
"Kadi ya China Union imejikita katika soko la China ambayo ina uwezo wa kumrahisishia mteja kuingia katika mfumo wa malipo ulio mzuri utakaowafanya wafanyabiashara wa Tanzania na wa China kufanya shughuli zao kikamilifu bila woga wowote juu ya upotevu wa fedha," alisema Kimei.Kimei alisema kuwa kadi hiyo itaweza kuwawezesha wateja wa benki ya CRDB kufanya malipo yake akiwa nchini China au Tanzania katika kufanya shughuli zake hasa za kibiashar

No comments:

Post a Comment