22 August 2013

KCB YAIPIGA JEKI HOSPITALI MOROGORO



Na Mwandishi Wetu, Morogoro
KUFUATIAo ng eze kokubwalawa gonjwawamoyokutokan ana ulajiwavyakula vin avyotengenezwaviwandani, uo ngoziwaHospi tali yaM koawaMorogoro umetoa wi tokwa jam ii nchinikutumiavy akulavya kiasili ili kuepukana naugonj wah uo
.Akizungu mzaM ko aniMorogorowakati wahafla yakuk abidhiwa mashin eyauchu nguzi wamoy okutokaB enk i yaKCBTanz ania, Ka imuMgangaMk uu waHosp italiyaRufa a Mkoa waMorog oroDkt. RitaLyam uy a amesema , jamii ikijie pushanamatumizi yavyakulavya kisasa idadi ya watu wanaopata matatizo ya moyo itapungua.
Akipokea msaada huo, Dkt. Lyamuya alisema mashine hiyo ilikuwa ni moja ya hitaji lao kubwa katika kukabiliana na ongezeko la wagonjwa waliokuwa wakihitaji huduma hiyo.Licha ya kupatiwa mashine ya 'Cardiac Monitor' kutoka Benki ya KCB Tanzania bado hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mashine za upasuaji na vitanda vya akina mama kujifungulia.
"Tunaishukuru Benki ya KCB Tanzania kwa kitendo cha kurudisha kiasi cha faida walichokipata kwa jamii inayowazunguka kwa kutununulia mashine hii, tunaziomba taasisi zingine zilizowekeza Morogoro kuiga mfano huu kwani kuchangia huduma za afya ni kuboresha maisha ya jamii," alisema Dkt. Lyamuya.
 Awali akikabidhi mashine hiyo, Meneja wa KCB Tanzania tawi la Morogoro Hogla Laizer alisema, wamefikia uamuzi huo baada ya kuona mahitaji ya wagonjwa wa moyo wanaofikishwa hospitalini hapo kutoka mikoa ya jirani yakiongezeka.
Akifafanua Hogla alisema, licha ya benki yake kuwahi kutoa msaada wa vitanda vya kujifungulia, mashine za upasuaji na Oxygen, mashine ya joto kwa watoto njiti Warm Incubator ongezeko la watu wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo liliwagusa na kuahidi kutoa msaada wa mashine hiyo.
"Matatizo ya moyo yamekuwa yakiongezeka kwa kiasi kikubwa katika kipindi hiki cha Sayansi na Teknolojia, msaada huu wa mashine ya kupimia moyo itasaidia kubaini mapema athari za maambukizi kabla hazijawa kubwa na hivyo kupunguza idadi ya vifo kutokana na ugonjwa huu," alisema Meneja huyo.
Hospitali zingine zilizofaidika na wiki ya Jamii inayoendeshwa na Benki ya KCB Tanzania Mwananyamala, Temeke, Buguruni, Mount Meru Arusha, KCMC Moshi na Mwembeladu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment