22 August 2013

JIJI KUONGEZA VITUO VYA MABASI YA MKOANI



HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam imetangaza kuwa mchakato wa kujenga vituo vya mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani katika maeneo ya Mbezi Luis, Boko Basihaya na Kongowe unaendelea vyema, anaripoti Hytham Mushi.

Mkuu wa Kitengo cha Uhifandi na Uhusiano wa Jiji, Gaston Makwembe aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Idara ya Habari (Maelezo).
Alisema kuwa, ujenzi wa vituo hivyo ni utekelezaji wa mipango ya jiji ya kuimarisha huduma ya usafiri jijini humo.
Alisema, Kituo cha Mbezi Luis kitahudumia wasafiri wa Kanda ya Kati na Nyanda za Juu wakati kituo cha Boko Basihaya kitatoa huduma kwa wasafiri wa Kanda ya Kaskazini huku Kanda ya Kusini Halmashauri ya Jiji itajenga Kituo cha mabasi Kongowe.
“Kutokana na upembuzi yakinifu wa awali, ujenzi wa vituo hivyo unakadiriwa kugharimu kiasi cha sh. bilioni 40 kwa kila kimoja, pia tunabaini vyanzo vya fedha na kuangalia uwezekano wa kuzishirikisha taasisi mbalimbali za fedha na wawekezaji wanaoonyesha nia ya kushirikiana na halmashauri ya jiji,” alisema.
Alisema, katika kipindi cha maandalizi ya ujenzi wa vituo hivyo, Kituo cha Mabasi Ubungo (UBT) kitaendelea kutoa huduma kwa wasafiri waendao mikoani na nchi jirani na baada ya kukamilika kwa ujenzi wa vituo hivyo, Kituo cha Ubungo kitakuwa kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi (DART

No comments:

Post a Comment