- GHOROFA LINGINE TISHIO HILI HAPA
- WAHUSIKA WAZIDI KUPIGA CHENGA
Na Goodluck Hongo
BAADHI ya maghorofa yaliyojengwa jijini
Dar es Salaam yamezidi kubainika kuwa ni tishio kwa wakazi wanayoyatumia,
wapita njia na majirani kutokana na kuwa na nyufa zinazoashiria kuwa yanaweza
kuanguka wakati wowote, huku mengine yakifikia hatua ya kuanza kuegemeana.
Uchunguzi
wa Majira jijini Dar es Salaam umefanikiwa
kubaini ghorofa lingine ambalo ni tishio kwa maisha ya wananchi, lakini cha
kushangaza mamlaka husika zimeendelea kukwepa kutoa ushirikiano, licha ya
gazeti hili hivi karibuni kuchapisha habari kuhusiana na hali ya ghorofa la Golden Plaza
lililopo kwenye mtaa wa Agrrey na Indira- Ghand.
Jengo
hilo la ghorofa takriban 10 lipo mtaa wa Zanaki
na Libya, jijini Dar es Salaam ambalo
limeyumba kiasi cha kugusana na ghorofa lingine.
Mmoja
wa maofisa katika Serikali ya Mtaa wa Kisutu, jijini Dar es
Salaam ambaye jengo hilo lipo kwenye
eneo lake la kiutawala, (jina tunalo) alisema hali ya jengo hilo wanaifahamu siku nyingi, lakini wahusika
ni Manispaa ya Ilala.
Alikiri
kuwa analifahamu jengo hilo,
lakini kitaalamu mhandisi wa Manispaaa ndiye anayeweza kulitolea ufafanuzi
zaidi ni kwa nini lipo katika hali hiyo.
Baadhi
ya wananchi wanaoishi eneo hilo, walisema kwa
muda mrefu jengo hilo
wamekuwa wakililalamikia lakini hakuna mamlaka husika ambazo zimeweza kuonesha
ushirikiano.
"Unajua
tatizo letu hapa ni uwajibikaji wa viongozi, watu wanasubiri hadi madhara
yatokee ndipo wawajibike, tumelalamika muda mrefu, lakini hatujaona
uwajibikaji," alisema na kuongeza;
"Majengo
haya tunayafahamu muda mrefu yalikuwa yameachana lakini sasa yamefikia hatua ya
kulaliana maana yake ni kwamba kama kusingekuwepo na jengo hilo (lililolaliwa) maafa yangetokea."
Gazeti
hili, lilishuhuda hali ya jengo hilo huku maisha
yakiendelea kama kawaida miongoni mwa wapangaji wa jengo hilo,
bila kujali hatari iliyopo mbele yao.
Diwani
wa Kata ya Kisutu ambaye ni Naibu Meya wa Manispsaa ya Ilala, Khery Kessy,
alipoulizwa kuhusiana na hali ya jengo hilo,
alisema wao sio wataalamu wa majengo bali wahusika wapo.
Alisema analijua suala hilo
tangu miaka minne iliyopita, lakini hadi
sasa hakuna
kitu kilichofanyika kwani kwa sasa hakuna mamlaka ya moja kwa moja ya
kushughulikia suala hilo.
"Zamani
jiji ndiyo lilikuwa linashughulika na kila kitu hata ambapo wao ndio wanunuzi
na waamuzi katika manispaa zao na hilo
lilikuwa rahisi hata kuwadhibiti watu ambao wanafanya makosa, lakini kwa sasa
hivi ni vigumu kwani kuna mamlaka nyingi zinazoshughulika na kitu kimoja na
matokeo yake ndiyo mengine yanajitokeza," alisema Diwani Kessy.
Alisema ni
vyema kila manispaa ziwe na mamlaka kamili ya kuiwezesha kudhibiti majengo ya
aina hiyo. Alitolea mfano hali ya chemba moja ya maji taka ambayo imeziba na
kumwaga vinyesi barabarani karibu na mitaa hiyo.
Alisema kila walipofuatilia
wahusika wanatupiana mpira, kila mtu anasema hahusiki, lakini kama Jiji
lingekuwa na mamlaka kama zamani hali hiyo
isingekuwepo na mara moja hatua zingechukuliwa.
B a a d h i y a wa s imami z i wa
majengo ya maghorofa waliozungumza na gazeti hili walisema mara nyingine hali
hiyo inatokana na kuchakachuliwa kwa ukubwa wa nondo au wakati wa kuchanganya
kokoto, saruji na mchanga (zege).
Walisema ujenzi wa ghorofa ambalo
baadaye linaenda upande husababishwa na kiti cha ghorofa kujengwa katika sehemu
ambayo haina mwamba mgumu.
"Kabla hujajenga nguzo za ghorofa
lazima kwanza uchimbe chini hadi ukutane na mwamba mgumu na hapo ndipo uanze
kujenga, lakini ukianza ujenzi katika eneo ambalo halina mwamba mgumu, basi
lazima jengo litaelemea upande mmoja na hatima yake ni kuanguka," alisema
mzee Mohamed Musa ambaye ni msimamizi wa ujenzi wa ghorofa nane.
Alisema ghorofa linaweza kuwa na nyufa
katika beem na likakaa kwa muda mrefu bila kuanguka lakini hiyo yote inatokana
na ujenzi ambao haukufuata viwango vinavyotakiwa.
Alisema mara nyingi nguzo
zinazoshikilia ghorofa lazima ziwe na nondo kuanzia milimita 25 na ziedelee
hivyo hadi sakafu ya mwisho, lakini ikiwemo nguzo moja kuwa na nondo 10 lakini
wengine huweka hadi milimita 16 hadi 20 na nondo nane katika beem moja na
matokeo yake ni kutokea ufa na wakati mwingine kuanguka.
"Mfano msikiti wa ...(anataja jina) una ufa katika beem na mimi
huo tangu miaka 10
iliyopita, lakini hadi leo unaendelea kutumika na sio hilo
tu bali kuna majengo mengi sana
hapa Kariakoo." alisema.
Gazeti hili lilifanya jitihada za
kuwasiliana na Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) Injinia Steven
Mlote, ili kuzungumzia suala hilo
lakini ilishindikana kutokana na Katibu Muhtasi kusema kwamba siku hiyo
asingeweza kuzungumza na mwandishi wa habari hii.
"Hautaweza kuzungumza naye kwani
haikuandikwa kwenye kitabu cha kumbukumbu (Kitabu cha watu wanaotakiwa kumuona
siku hiyo,) alisema Katibu Muhutasi huyo.
Awali gazeti hili liliwasiliana na
Injinia Mlote kwa njia ya simu ambapo alimtaka mwandishi aende ofisini kwake
ili azungumzie suala hilo,
lakini alipoenda hakuweza kuonana naye.
Pamoja na Katibu Muhutasi kuelezwa
hivyo, bado aliendelea kushikilia msimamo kuwa wanaoingia kumuona ni wale wenye
miadi naye.
Gazeti hili lilipomtafuta Mhandisi wa Manispaa ya Ilala ili kuzungumzia
suala hilo kila
wakati alikuwa akidai yupo kwenye shughuli zingine au kwenye vikao
Majanga haya yatatuandama daima kama wahusika hawatachukuliwa hatua za kisheria - inaonekana kuwa kuna ulaji mkubwa baina ya NHC, maafisa wa serikali na wale wanaojiita wawekezaji - matokeo yake majengo haya yataporomoka na kuwaua wengi - Ndo maana waziri anatoa amri ya kubomolewa lakini hakuna anayejali
ReplyDeleteTanzania tuna kazi kubwa sana kufikia maendeleo endelevu,hakuna uwajibikaji kwa wahusika,kila kitu ni vululu vululu tu,sijui hadi wafe wajmba zao wa damu ndo wawajibike, hivi sie aliyeturoga kafa nini ndo maan kila sehemu hakuna kinachowezekana kufanikiwa,Serikali kazi yake ni nini,watendaji nao kazi zao ni nini,mbona majangaa,loh!!
ReplyDelete