Cresensia Kapinga
WATU wanne wa familia moja wamefariki na wengine 13
wamelazwa hospitalini kutokana na kula chakula chenye sumu wakati wa sikukuu ya
Idi el Fitri.Watu hao wamelazwa Kituo
cha Afya cha Lusewa wilayani Namtumbo na Hospitali ya Serikali ya Mkoa wa Ruvuma (HOMSO).
Kamanda wa Polisi Mkoa
Deusidebit Nsimeki, alisema tukio hilo
lilitokea Agosti 9, mwaka huu saa 7:00. Kamanda Nsimeki, alisema siku hiyo
kabla ya tukio, Salum Mumba, alinunua samaki aliyepeleka nyumbani kwa ajili ya
sikukuu ya Idi.Kamanda Nsimeki alisema k a
t i k a t u k i o h i l o P o l i s i wanamshikilia mtu mmoja ambaye hakutaka
kumtaja jina ambaye atasaidia polisi kwenye upelelezi wake.
Alisema baada ya kula
chakula hicho, haikuchukua muda mrefu mtoto alianza kuumwa naye baadaye
alifariki dunia. Baadaye watoto wawili walianza kuumwa na kufariki. Watu
wengine 13 walianza kuumwa baadaye majirani walipata taarifa kuwakimbiza watu
hao hospitali.
Aliwataja waliolazwa katika
kituo cha afya cha Lusewa kuwa ni Tazamio Mumba, Zidani Mumba, Ramadhani Mumba
na Zahara Mumba wote wakazi wa kitongoji Tulieni B.
Waliolazwa katika hospitali
ya Mkoa wa Songea kuwa ni Gairi Mumba, Zamoni Mumba, Fatuma Rashidi, Samidu
Mumba, Asha Omary na Sharifa Mumba.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi ya Hospitali ya Mkoa Songea Dkt.
Benedictor Ngaiza alisema wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo hali zao zinaendelea
vizuri.
No comments:
Post a Comment