13 August 2013

FUESA ZA BIASHARA KUONGEZEKA MTWARAMKOA waMtwar aumezidi kupataf ursa nyingiza biasharakw a kuto kananau amuziwaB ankofAf ricaTanz ani akufung ua tawi lakeji pya k atikamkoahuouliokusi nimwaTanz ania, a nari poti Mwandishi Wetu, Mtwara. Tawi hilo nila 19kufunguliwa na benki hiyo h ap a nc hini. N aibu M kurug enzi Mtendaji wabenk ihiyo,EricOuattaraaliwaambi awaand ishi w a hab ari jana mjiniM twarakuwahatuayakufun gua ta wihilo inae ndananakaulimbiuya mwakaya ben ki hi yoambayo ni kuendeleza Bara laAf rika.

Alis ema,Mko awa Mtw araambaoumeja liwaar dhin zurikwa kilimocha koro sho,ban darinakupatik anakwagesi namafu ta, unahitaji hudum a zakifedhaambazozitawezeshawaj asiriam ali na kampu nikat ikae neo hilokutumia vyemafu rsahiz ozau chum i.
"Mtwar ainahitaji hud umaza kibenki iliku wezeshaw atukutum iavizurifurs azinazo pa tikan a hapahasa ka tikam aeneoyagesi,mafuta, bandarina kilimo cha korosho," alisema.
Alisema benki imeanzisha huduma maalum mbalimbali zitakazosaidia kufanikisha hilo.
Alitaja baadhi ya huduma hizo kama mikopo kusaidia biashara na ujenzi, kupatikana kwa vifaa na mashine mbalimbali pamoja na huduma nyingine zitakazopatikana kwa gharama nafuu.
Alizitaja huduma nyingine kama kutoa garantii na huduma za ulipaji fedha kimataifa na huduma za kielektroniki za benki.
Bank of Africa Tanzania ilianza huduma zake zaidi ya miaka 30 iliyopita huko Bamako, Mali.
Hadi sasa benki hiyo ina mtaji wa zaidi ya Euro 3.85 bilioni.
Kwa hapa nchini, benki hii ina zaidi ya miaka saba ikihudumia makampuni makubwa pamoja na kada ya wajasiriamali wadogo na wa kati.
Kwa sasa ina matawi katika mikoa ya Dar es Salaam (yenye matawi kumi) na mengine katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Mtibwa, Mbeya, Tunduma, Mwanza, Kahama na sasa Mtwara.

1 comment:

  1. hivi mhariri umeona na kuipitia habari hii?

    ReplyDelete