Goodluck Hongo na Revina
John
JESHI
la Polisi nchini kwa kushirikiana na Idara ya Wanyamapori limemkamata r a i a w
a U i n g e r e Robart Dewar (64), akiwa na nyara mbalimbali za Serikali ikiwemo
meno ya tembo nane yanayokadiriwa kuwa na thamani ya sh.milioni 118.4 Raia huyo
pia anadaiwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trans Africans Ligostics Limited
(TALL) hapa nchini.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam
jana iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, SSP Advera Senso
ilieleza kuwa mtuhumiwahuyo alikamatwa Agosti 9, 2013 saa 2:30 usiku huko Mbezi
Beach akiwa na nyara hizo yakiwemo pia meno ya simba 20 na kucha 22. Taarifa
hiyo ilifafanua kuwa, mtuhumiwa alikamatwa na nyara hizo zikiwa na uzito wa
kilo 24 na vinyago vilivyotengenezwa kwa meno ya tembo 11 pamoja na ganda moja
la bomu lenye ukubwa wa milimita 130.
Alisema, mbali na kukamatwa na nyara hizo lakini pia mtuhumiwa huyo
alikamatwa na shanga mbalimbali 15 zilizotengenezwa na meno ya tembo ikiwemo pia
ndege mmoja aina ya kasuku. “Tumemkamata raia wa Uingereza akiwa na nyara za Serikali,
vikiwemo vipande nane vya meno ya tembo, vinyago 11 vilivyotengenezwa kwa meno
ya tembo, meno 20 na kucha 22 za Simba, shanga 15 zilizotengenezwa kwa meno
ya Tembo, ndege mmoja aina ya kasuku, vipande vya miti ya mpingo.“Na
idadi kubwa ya vinyago ambavyo haviruhusiwi kumilikiwa na mtu yeyote bila
kibali cha Idara ya Misitu, ganda moja la bomu lenye ukubwa wa milimita 130 na mawe
mbalimbali yanayodhaniwa kuwa ni madini,”alisema SSP Senso. Alibainisha kuwa,
mtuhumiwa huyo alikamatwa kutokana na wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la
Polisi kwa kuwaambia
kuwa mtuhumiwa huyo anamiliki nyara mbalimbali za Serikali nyumbani
kwake na wakati mwingine huzisafirisha sehemu mbalimbali duniani na ndipo walipomfuatilia
na kumtia mbaroni.Aliongeza kuwa, mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara
baada ya upelelezi wake kukamilika na kuwaomba wananchi kuongeza kasi ya kutoa taarifa
za uhalifu na wahalifu ili kukomesha biashara haramu ya usafi rishaji wa nyara
za Serikali. Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la watu
kukamatwa na meno ya tembo ikiwemo ndani na nje ya nchi hali inayoendelea
kuhatarisha kutoweka kwa wanyama hao kutokana na kuuawa kwa kasi kubwa na meno
yake kusafi rishwa nje ya nch
Anatafuta utajiri wa haraka. Wakamateni pia walio muuzia. Uroho kazi yake ni kuumia. Kaumia tayari huyo.
ReplyDeletemaskini simba na tembo wetu. naona wamnajuta kuzaliwa bongo manake nchi hii full michosho.
ReplyDelete