Gladness
Theonest na Theophan Ng'itu
RAIS wa Chama cha
Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, amesema matokeo mabaya ya walimu
yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) hayawashangazi kwani
walishaiambia Serikali iwe inapeleka vyuoni wanafunzi wenye ufaulu mzuri,
lakini haifanyi hivyo.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Mukoba alipozungumza na Majira. Alisisitiza kuwa
pamoja na kupigia kelele suala hilo, lakini Serikali imekuwa ikiendelea
kupeleka wanafunzi wabovu, hivyo imevuna ilichopanda.
Al
i s ema ma t o k e o h a y o pia yamechangiwa na Serikali kutosikiliza madai
yao kwani tangu mwaka jana walimu na Serikali wamekuwa na ugomvi usiokuwa na
majibu.
Aliongeza
kuwa madai ambayo walikuwa wakiyadai ni pamoja na nyongeza ya asilimia 100 ya
posho ya kufundishia, asilimia 50 ya mazingira magumu, lakini hadi sasa
wamepewa nyongeza ya asilimia 8 tu ya nyongeza ya mshahara.
Mukoba alisema walimu
wa vyuo ambao ndiyo wana kazi kubwa ya kufundisha walimu ndiyo waathirika
wakubwa kutokana na kutopandishwa vyeo, kutokurekebishiwa mishahara, kutopata
fedha za mizigo, likizo na matibabu, ukichanganya hali hiyo inasababisha ufaulu
mdogo.
"Ukipanda ujinga
unalima uzuzu, sio mara ya kwanza hali hii inatokea, Serikali imeendelea kuziba
masikio kwa suala nyeti kama hili la elimu, huku ukitarajia taifa kwenda
mbali," alisema Mukoba.
Alisema madhara ya
hali hii ya matokeo mabaya ya ualimu jamii haitakuwa na imani na walimu na hata
yule ambaye alikuwa anatamani kuingia katika fani ya ualimu hawezi kutamani
tena.
Mukoba aliongeza kuwa
damu ya taifa ni elimu na pindi inaposimama taifa litakufa, hivyo lawama zote
ipewe Serikali kwani imekuwa ikipewa ushauri wa kutosha lakini imekataa
kuupokea.
"Nina imani hata
katika matokeo haya hawatachukua hatua sahihi, zaidi wataunda tume ambayo
itatoa matokeo wanayoyajua tayari na sisi kama CWT hatuwezi kuridhika na
kukubali Taifa lididimie mikononi mwetu, lazima tuchukue hatua hata kama hatua
hizi hazitakuwa na chembe ya utamu," alisema Mukoba.
Majira ilizungumza na baadhi ya walimu ambao hawakutaka
kutaja majina yao
gazetini walisema kuwa katika matokeo hayo hakuna kipya, kwani hicho
kilichotokea ndicho walichokuwa wanakitarajia
NINARUDIA KUSEMA KWAMBA shetani amevamia elimu ya kitanzania na kufaulu ENYI KINA NDALICHAKO,KAWAMBWA,NA WENGINE SIMAMIENI NA KUHAKIKISH PALE MNAPOSHINDWA SHIRIKIANA NA WENGINE NA KAMA KUNA MIGOGORO SAIDIENI IONDOKE MAANA HAO WALIMU NI WAMINIFU WAMEKUBALIANA KUNIA MAMOJA NA VIONGOZI ILA EPUKENI MIZENGWE KAMA MNAWAPA AHADI ZITIMIZENI ILI TUFIKIE LENGO NDG ZANGU TUFIKE WAKATI TUAMUWE KUJIKOMBOA KIELIMU ILA BADO ELIMU INAYOTOLEWA IKIDHI VIWANGO
ReplyDelete