24 August 2013

ALIYEMSHTAKI LIYUMBA AGONGA MWAMBA



Na Rehema Maigala
MAHAKAMA ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, jana imetupilia mbali ombi la Bi. Aurelia Ngowi, aliyekuwa mke wa Mkurugenzi wa Utawala na Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Amatus Liyumba
.
Bi. Ngowi alifungua kesi mahakamani hapo akitaka aruhusiwe kuishi katika nyumba iliyopo Mbezi Beach ambapo ombi hilo lilitupwa baada ya mahakama kwenda kujiridhisha katika nyumba hiyo na kukuta ni ya biashara si ya kuishi familia kama alivyodai katika maombi yake.Hata hivyo, mahakama hiyo imemtaka Bi. Ngowi ahame katika nyumba hiyo ili mdaiwa Bw. Liyumba aendelee na shughuli zake za kibiashara.
Kesi hiyo ilikuwa mbele ya Hakimu Jackline Rugemalila, ambaye alidai kuwa, hayo ni ma omb i ma d o g o amb a y o yalipelekwa na mdai mahakamani hapo.Mahakama hiyo ilikwenda hadi katika nyumba husika ambapo baadhi ya majirani walisema nyumba hiyo tangu ijengwe, haijawahi kuishi watu bali ni nyumba ya biashara Amjen Excutive Hotel.
Bi. Ngowi alipeleka maombi saba mahakamani hapo ambayo ni kuiomba mahakama hiyo imzuie Bw. Liyumba aache kutawanya mali za familia pamoja na kutaka kuuza nyumba inayokaa familia.
Katika kesi hiyo ya madai, Bi. Ngowi alidai kufunga ndoa na Bw. Liyumba mwaka 1978. Kesi ya msingi ya madai ya talaka, itatajwa Septemba 16 mwaka huu.Bw. Liyumba anatetewa na wakili Sweetbert Nkuba wa kampuni ya Austin and Wilson, wakili wa mdai ni Margaret Ringo

No comments:

Post a Comment