24 August 2013

KORTINI KWA KUFOJI SAINI YA PINDA



Na Rehema Mohamed
MFANYABIASHARA Ahmed Popi (35), jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, akikabiliwa na shtaka la kufoji barua na saini ya Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda.
Mbele ya Hakimu Waliyarwande Lema, wakili wa Serikali Hamisi Saidi, alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo muda na terehe isiyofahamika jijini Dar es Salaam.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, mshtakiwa huyo alifoji barua yenye kumbukumbu namba DA 21/2078/01A/142 ya Desemba 3, 2012 kwa lengo la kuonesha ni halisi iliyotolewa, kusainiwa na Waziri Mkuu Bw. Pinda.Katika shtaka lingine, ilidaiwa mshtakiwa huyo kwa lengo la kudanganya katika tarehe hizo, bila ya kupata ruhusa ya mamlaka husika alifoji na kusaini barua hiyo.
Ilidaiwa kuwa, mshtakiwa alifoji barua hiyo kwa lengo la kumpelekea Islam Mtila na kuonesha kuwa imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu wakati akijua si kweli.Mshtakiwa alikana kutende makosa hayo na amerudishwa rumande baada ya kukosa wadhamini. Hakimu Lema alimtaka mshtakiwa awe na wadhamini wawili ambao watasaini bondi ya sh. milioni 10 kila mmoja. Sharti lingine ni kuwa na mdhamini mmoja kati ya hao ambaye atasaini hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo. Kesi imeahirishwa hadi Septemba 5 mwaka huu, itakapotajwa

No comments:

Post a Comment