24 August 2013

CUF WAMVAA NCHIMBI

  • WAIBANA SERIKALI VIGOGO DAWA ZA KULEVYA


Na Darlin Said
CHAMA c h a Wa n a n c h i (CUF), kimemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi, kukomesha biashara, matumizi ya dawa za kulevya na utoroshaji wa nyara za Serikali.Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba, aliyasema hayo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana wakati akizungumzia maazimio ya Baraza Kuu la CUF Taifa, ambalo liliazimia mambo mbalimbali.

Alisema jukumu la kukomesha vitendo hivyo nchini, halipaswi kufanywa na Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe ili kuwalinda vijana na heshima ya Taifa.A l i o n g e z a k u w a , D k t . Mwakyembe ana majukumu mazito ya kusimamia reli, bandari, viwanja vyndege, usafirishaji pamoja na suala zima la uchukuzi.
Prof. Lipumba alisema, umefika wakati wa Serikali kupambana na wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya ambao ndiyo wanaoharibu sura ya nchi kimataifa badala ya kuelekeza nguvu zao kwa wafanyabiashara wadogo.
"CUF inasikitishwa na biashara ya dawa za kulevya kushika kasi nchini na kutoroshwa kwa nyaraka za Serikali bila vyombo vya dola kuchukua hatua stahiki badala yake nguvu kubwa inatumika kuzima uhuru wa vyama vya siasa, waandishi wa habari, wanaharakati na viongozi wa dini."Nguvu hizi zingetumika kupambana na majanga ya ujambazi, wizi wa rasilimali, ubadhirifu serikalini na madhambi mengine,
Watanzania wangekuwa na uchumi imara na kungejenga Taifa lenye nguvu kubwa kidemokrasia siku za usoni," alisema.Wakati huo huo, baraza hilo limedai kusikitishwa na mgogoro wa kiuchumi uliotangazwa na nchi za Rwanda na Uganda juu ya kutumia Bandari ya Dar es Salaam kutokana na urasimu uliopo pamoja na miundombinu mibovu ya barabara, bandari.
"Baraza limeitaka Serikali kulitazama jambo hili katika sura ya kiuchumi badala ya mtazamo wa kisiasa ili kuweka mkakati wa kulinusuru Taifa," alisema Prof. Lipumba.Alitoa wito kwa Rais Jakaya Kikwete, kuendelea kutumia njia za kidiplomasia kutatua mgogoro uliopo kati ya Tanzania na Rwanda ili kuleta maelewano ambayo yatadumisha usalama wa nchi hizo.
Katika hatua nyingine, CUF imeitaka Serikali itoe taarifa zinazohusu ripoti za uchunguzi uliowasilishwa na tume zilizokuwa zikichunguza matukio mbalimbali ili wananchi waweze kujua ukweli.Alizitaja tume hizo kuwa ni pamoja na ile ya kuchunguza mauaji ya Padre Mushi, Mwandishi Daudi Mwangosi, kutekwa na kuteswa kwa Dkt. Ulimboka, Mhariri Absalom Kibanda na kuitaka iunde tume huru ya kuchunguza tukio la kupigwa risasi kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shekhe Ponda Issa Ponda

 

No comments:

Post a Comment