04 July 2013

WINDS YAFURAHISHWA NA OBAMA


KAMPUNI ya kuzalisha umeme ya Wind East Afrika imefurahishwa na kitendo cha Rais wa Marekani, Barack Obama kwa kuijumuisha kampuni yao katika mpango wa kuondoa tatizo la nishati ya umeme kwa nchi zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara, anaripoti Darlin Said.
Mpango huo uliotangazwa rasmi Juni 30, mwaka huu na Ikulu ya Marekani, unatarajia kuzalisha umeme wa megawatt 400 mkoani Singida na kuwa mradi mkubwa wa kwanza nchi za Kenya na Tanzania kwa gharama ya uwekezaji wa dola za kimarekani bilioni 1.1.
Ikulu ya Marekani ilitoa orodha ya miradi ya umeme kwa nchi hizo na kuitaja kampuni mshirika wa Wind East Africa, ijulikanayo kwa jina la Aldwych International kuwa miongoni mwa makampuni ambayo yatapata misaada kwa ajili ya kuongeza kasi ya kukamilisha kwa mradi wa umeme wa upepo wa Singida kwa matumizi ya hapa nchini.
Mbali ya Tanzania, nchi nyingine ambazo zitafaidika na mpango huo ni Ethiopia, Ghana, Kenya, Liberia na Nigeria. Mpango huo una malengo ya kurahisisha uwekezaji na uzalishaji katika nchi hizo. Mradi wa Power House pia upo kwa nchi za Uganda na Msumbiji kwa kutumia umeme wa mafuta na gesi.
Nchi ya Marekani imewekeza kiasi cha zaidi ya dola za kimarekani bilioni 7 kwa mpango wa miaka mitano ijayo ya kuwekeza katika nishati ya umeme.
Mwasisi na Mkurugenzi wa Mradi huo, Rashid Shamte alisema jana kuwa kuwemo katika mpango wa Ikulu ya Marekani na Rais Obama katika mpango huo ni faraja kubwa kwao kwani nia yao kubwa ni kuondoa tatizo la umeme hapa nchini.
ìKwa kweli tumefurahi sana kuwepo katika mpango wa Ikulu ya Marekani (White House) na Rais Obama, hii ni faraja kwa Watanzania kwani kwa kipindi kifupi kijacho, wataanza kufaidika ma matunda ya mradi huo wa uzalishaji wa nishati ya umeme,î alisema Shamte

No comments:

Post a Comment