04 July 2013

DOLA BILIONI 2.5/- KUTOLEWA BURE KUCHANGIA UMEME AFRIKA



 Na Jamaal Mlewa
KAMPUNI ya HEIRS Holdings imeahidi mchango wa dola bilioni 2.5 kati ya dola bilioni saba ambazo serikali ya Marekani imeahidi katika kufadhili utekelezaji wa mradi wa umeme unaojulikana kama 'Power Afrika.'
Hayo yalibainishwa juzi na Mwenyekiti wa HIERS Holdings, Tony Elumelu wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Elumelo ni mfanyabiashara raia wa Nigeria ambaye amepata mafanikio makubwa katika sekta ya mafuta.
Alisema, mradi huo unalenga mambo mawili m a k u b w a i k i w a n i kuhakikisha idadi ya watu wanaopata umeme inaongezeka maradufu lakini pia kuziwezesha nchi za Afrika kujenga uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha.
Pamoja na dola bilioni saba alizoahidi Rais Barack Obama, taasisi mbalimbali binafsi nazo zimetoa dola bilioni tisa ili kufanikisha mradi huo utakaonufaisha nchi za Tanzania, Kenya, Liberia, Nigeria, Ethiopia na Ghana.
Awali akizindua mradi mk u b w a w a umeme unaotekelezwa na Kampuni ya Symbion Power, Rais Barack Obama ameitaka serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa miradi iliyopangwa kutekelezwa chini ya ufadhili wa Marekani haicheleweshwi bila sababu za msingi.
"Kwa k u a n z i a , i l i k u t e k e l e z a d h ami r a yetu, tutahakikisha kuwa tunawapatia umeme watu milioni 20 katika nchi sita ambako mradi utatekelezwa," alisema Rais Obama.
Hata hivyo, takwimu zinaonyesha kuwa takribani watu milioni 600 kati ya wakazi bilioni moja barani Afrika hawana umeme.
Mradi huo umekuja wakati ambapo serikali ina mkakati wa kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka kiwango cha sasa megawati 1,438.24 hadi kufikia megawati 2,780 mwaka 2015.
Kampuni ya Symbion Power ambayo inaelekea kuwa mkombozi wa kero ya nishati ya umeme nchini ilinunua mitambo ya Dowans mwaka 2011.
Dowans mpaka sasa ina mgogoro na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) ikidai kiasi cha dola milioni 65 ambazo iliamriwa kulipwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi ya Biashara.
Dowans ilirithi mitambo hiyo kutoka kwa Kampuni ya RICHMOND ambayo ilituhumiwa na Bunge kuwa na uwezo mdogo wa uzalishaji umeme mwak 2007.

No comments:

Post a Comment