27 April 2011

Mafisadi CCM waandaa mamilioni kujisafisha

*Wadaiwa kuandaa vijana kupinga hatua dhidi yao

Na John Daniel

KUNDI la mafisadi wanaokabiliwa na hatihati ya kuvuliwa uongozi na pengine uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamebuni mbinu mpya
kujihami kwa kutumia haramu kwa kuandaa vijana kufanya maandamano kumpinga Rais Jakaya Kikwete na chama chake.

Kundi hilo linapinga vikali uamuzi wa CCM kupitia Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), kuwapa muda wa kujiengua wenyewe kabla ya kufukuzwa baada ya siku 90.

Habari za uhakika kutoka vyanzo vyetu vimeeleza kuwa kundi hilo limepitisha bajeti ya mamilioni ya fedha kwa ajili ya kuwandaa vijana kufanya maandamano kupinga uamuzi wa kuondolewa NEC na hata CCM kwa ujumla, mara tu baada ya kukabidhiwa barua muda wowote kuanzia wiki hii.

"Tayari wameapa kuwa wakiondolewa ni lazima Rais Kikwete naye aondoke kwa kuwa ndiye aliyepitisha maamuzi ya kuwafukuza, wanapanga vijana kwa kuwarubuni kwa fedha haramu ili waandamane mara tu watakapopewa barua.

"Wiki iliyopita walikutana wakapitisha zaidi ya milioni 500 kumshughulikia Bwana mkubwa (Rais Kikwete), wanataka kumchafua ili kummaliza nguvu kuwashughulikia," kilisema chanzo kingine.

Habari hizo zilieleza kuwa mbali na Rais Kikwete anayeelezwa na kundi hilo kukabiliwa na tuhuma na ufisadi, akiwa miongoni mwa watu 11 waliotangazwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa, na familia yake, akiwamo mwanawe Ridhiwan anayedaiwa kuwa mali kuliko kipato chake, pia kundi hilo linasaka kwa udi na uvumba majalada ya mawaziri wanne wa sasa kwa lengo la kuwaunganisha katika tuhuma za ufisadi,  kwa kinachoelezwa kuwa ni kampeni ya 'tuchafuke wote'.

"Kati ya fedha hizo sh. milioni 18 zitatumwa katika mikoa 20 kugawiwa vijana ili wafanye maandamano ya kupinga kuondolewa na kuwapakazia wengine wanaotaka waondoke nao kama njia ya kujitakasa.

"Fedha zinazobaki zinatumika kununua mafaili ya watu wengine kutafuta makosa yao ya aina yoyote akiwamo Waziri wa Afrika Mashariki, Bw. Sitta (Samwel) Prof. Mwandosya, (Mark), Dkt. Mwakyembe (Harrison) na Membe au Magufuli," kilisema chanzo chetu.

Ilielezwa kuwa kundi hilo limekuwa likifanya vikao katika maeneo maeneo mbalimbali kwa lengo la kutaka kujisafisha na ufisadi, au kupunguza makali kwa kutaja wengine.

"Mmoja wao amejiandaa kuzungumza na waandishi wa habari kuwapa nyaraka za uongo ili kuwachafua watu wengine, walengwa wakuu ni Rais na familia yake, mawaziri wanne na wengine wadogo," kilisema chanzo kingine.

"Usifikiri hatujui hayo, mbinu zote wanazofanya tunazijua, hatuwezi kupambana na wajinga, tunasubiri tuone mwisho wao, lakini hata ninyi waandishi lazima mjue kuwa Watanzania wanaosoma vitu mnavyoandika wanajua yote," alisema kigogo mmoja wa serikali bila kutoa ufafanuzi.

Mbinu nyingine iliyotajwa mara baada ya uamuzi wa NEC Dodoma ni kuwatumia viongozi wa vyama vya siasa kutoa tuhuma mpya ili ionekane kwamba wameonewa na kupoteza lengo la kuwaondoa.

Pamoja na kwamba hakutaja jina, Chama cha demokrasia na Maendeleo ndicho kimetaja watuhumiwa wapya wa ufisadi, huku Katibu Mkuu wake, Dkt. Slaa akipinga madai ya kutumiwa kufanya hivyo kwa nia ya kuwachafua.

Katika tuhuma hizo, alizungumzia uuzaji wa nyumba za serikali bila kufuata utaratibu zilizoelekezwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na aliyekuwa waziri wake wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli; Kuhusu fedha za EPA na mahali zilipo zile zilizorejeshwa akielekeza tuhuma hizo kwa Rais Kikwete na John Malecela na Philip Mangula waliodaiwa kuhusika katika wizi wa fedha za EPA, hasa zile zilizoingia katika kampeni ya CCM mwaka 2005.

Katika hatua nyingine kundi hilo la mafisadi wa linadaiwa kuwalenga baadhi ya viongozi wa dini kuwasafisha kwa kutangaza msimamo kuwa wameonewa na hakuna mtakatifu au wao wametolewa kafara.

Majira ilipomtafuta Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Bw. Nape Nnauye kujua kama wana taarifa hizo alikiri na kuongeza kuwa haziwasumbui kwa kuwa mfa maji hakosi kutapatapa.

"Kwanza nilishasema nilipokuwa uwanja wa Manzese, niliwaambia wananchi kuwa mafisadi wamejipanga kumchafua Mwenyekiti wetu na familia yake.

7 comments:

  1. Mh.Nape huna jipya ww kaa ule pesa za Chama uende zako.Mfupa ulioshinda fisi ww utauweza?
    Ukumbuke kuwa Mafisad ndio walioingiza CCM madarakani.Sina uhakika kama Mh.Nape unaweza kuumnyoshea mkono Mh.Rostam.

    ReplyDelete
  2. HISTORIA HIPO PALEPALE SEMENI YOTE MAANA NYIE MLISOMESHWA NA SERIKALI UJASUSI URUSI ZAIDI YA MIAKA 7 NA WENGINE WALISOMEA UJASUSI MIAKA 14.PANGENI HOJA ZA KUJISAFISHA LAKINI WANANCHI WANAJUA

    ReplyDelete
  3. Hiyo ni danganya toto. Wanabebebana hao na raisi wao pamoja na familia yake. Ni wezi watupu na mungu atakuja kuwahukumu kwani ni watanzania wengi wanaoteseka kwa umasikini walio, nao wao wanachezea pesa "vijisenti kwao" jinsi wanavyotaka.

    ReplyDelete
  4. HIVI CCM INATAKA IWADANGANYE WAKINA NANI? KWANINI NAPE ANASEMA KWAMBA WAMEPANGA KUMCHAFUA KIKWETE? KIKWETE AMEJICHAFUA MWENYEWE NI FISADI YEYE NDIYE ALIYEBUNI MBINU YA KUIBA PESA EPA NA KUTENGENEZA KAMPUNI YA KAGODA...CCM NI WANAFIKI NA WAONGO,SIKU ZOTE WALISEMA CCM HAKUNA MAFISADI,HATA KIKEWTE ALITUMIA ALIWAINUA MIKONO KWAMBA NI WASAFI.LEO WANATAKA KUDANGANYA WATU KWAMBA WANASHUGHULIKIA MAFISADI WAMETOKA WAPI? KAMA KIKWETE ASINGEKUWA FISADI ANGESHAWAKAMATA MAFISADI WOTE NA KUWAFUNGA.KUDAI KUWA MAFISADI WANATUMIA VYAMA VYA UPINZANI NI UONGO.

    ReplyDelete
  5. Jamani kwa kweli hapa nchini wengi sio wasafi hata walio chini wengi sio waaminifu sema tu hao wamejulikana. Tena utakuta wanaoshabikia ndio wenyewe haswaa! wa kisirisiri ila tu hawajawekwa hadharani kama hao wanaoandamwa baada ya kujulikana. Hata kwenye ofisi mbalimbali watu ni mafisadi ile mbaya. Dhambi ni dhambi tu hata ikiwa ni ndogo.

    Nimesoma kwenye biblia kuwa kuna mwanamke alipelekwa kwa Yesu kwa ajili ya uovu wake. Baada ya kufikishwa kwa Yesu wakaambiwa wale waliotaka kumwadhibu kwa mawe kuwa, anayejiona ni msafi achukue jiwe na awe wa kwanza kumpiga. wote walikimbia baada ya kujiona nao ni waovu pia. Tatizo la sisi binadamu tunapenda sana kunyooshea wengine vidole wakati sisi pia ni waovu kupindukia.

    Ushauri wa kuiokoa nchi yetu:
    Watu tutubu kwa makosa yetu hata hao walioshtakiwa watubu hadharani na tuwasamehe tuanze upya kuijenga nchi yetu. Maana kwa mwendo tunaokwenda utakuwa ni mwendo wa visasi, kumwagiana tindikali na kuuana tu. NAIPENDA NCHI YANGU NA WATU WAKE PIA. ILA MWENDO TUNAOKWENDA NAO UNANITIA UCHUNGU SANA.

    ReplyDelete
  6. n kwel kuwa hamna alye msaf ila kumbuken kuwa mfumo wa uongoz unapoharbka ndipo chn kunadoda.tunahtaj mfumo a juu ulio imara utakaowajbsha wote. kikwete ameshndwa kaz

    ReplyDelete
  7. JAMANI TUWE WAVUMILIVU NA WAKOMAVU WA KISIASA, KWANUI WAO WAMEAMBIWA MAFISADI AU WANATUHUMIWA KUWA MAFISADI? NA KWANINI ULALAMIKE KAMA KWELI UMSAFI? TUIONEE HURUMA NCHI YETU NA 2KIONEE HURUMA CHAMA CHETU CCM PIA. JAMANI TUACHENI UNAFIKI, WALIOPITISHA MAAZIMIO AKINA NANI? HAO WENGINE SI WALIKUWAPO? WALIHOJI KTK KIKAO? AU NDO TEGEMEO LAO PESA? TUTAMBUE PENYE UKWELI UWONGO UTAJITENGA, TUBADIRIKE SASA. NAWAONEA HURUMA HAO VIJANA WATAKAO TUMIWA, KWANI HAWATAONA HAIBU KUTUMIWA NA ASIOWAJUA? NAWASHAURI WAKIPEWA PESA WALE NA WAWAOMBE WAO MAFISADI WATANGULIE MBELE AU WATOTO WAO TUWAONE KTK MAGAZETI. TUKUMBUKE WAKATI HUU NI WAKATI WA KUFIKIRI KWA KICHWA NA SI KWA TUMBO TENA. MUNGU IBARIKI TANZANIA SALAMA TUYORITHI TOKA KWA MAREHEM NYERERE, MUNGU IBARIKI CCM.

    ReplyDelete