26 July 2013

WAZANZIBARI WAHOJI MUUNGANO KORTINI



 Na Mwajuma Juma, Zanzibar
MAHAKAMA Ku u y a Zanzibar imeahirisha kesi ya kikatiba ya kudai uhalali wa kuwepo kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa mwaka 1964.Kesi hiyo iliyokuwa chini ya Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, George Kazi, ilifunguliwa na Wazanzibar 1,950. Katika kesi hiyo Serikali inawakilishwa na Mark Mulwambo na wadai wanatetewa na wakili wa kujitegemea, Philip Ojode, ambapo ilitajwa mahakamani hapo jana.

Mrajisi huyo alisema kutokana na mhusika wa kusikiliza kesi kutokuwepo mahakamani inaahirishwa hadi Agosti 23, mwaka huu. Wazanzibari hao wanaongozwa na Rashid Salum Adiy, ambaye alianza harakati za kudai uhalali wa Muungano tangu mwaka 2005.
Harakati hizo za kudai uhalali wa Muungano huo zilianza huku kundi hilo likiwa na watu 10 (G10), ambao walifungua shauri kwenye mahakama Kuu ya Zanzibar wakitaka Mahakama imuamuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwasilisha mbele ya Mahakama hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar..  

4 comments:

  1. hawa wanaohoji muungano ni akina nani na wanamaslahi gani katika hili, siyo wanatumiwa na mabwana zao walopo nje? kwanini hawakuhoji kipindi hicho muungano unaundwa? au ni vipandikizi vya uzanzibari hawa? Tusipoziba ufa tutajenga ukuta na huo ukuta utakuwa haujengeki tena. waangalieni hawa wanaotaka kuhoji kitu ambacho kipo wazi.Muungano wetu ni mfano wa kuigwa na kupigiwa mfano huyo Rashid Salum Adiy ni nani?

    ReplyDelete
  2. Muungano uliopo ni haki kuhojiwa ili ipatikane ithibati ya uhalali wake tuwache tabia ya kuvungavunga ukweli na kupelekea kupotea hali za wazanzibari kitaifa na kimataifa, pia sio kosa(uharamu) katika kutaka kuelewa uhalali wa muungano, watanzania wenzangu tuacheni ubabaifu na kutishana katika demokrasia, waacheni wazanzibar waamue mbona sisi tunasmua.
    Ahsanteni

    ReplyDelete
  3. Ndugu yangu nakupongeza kwa kumueleza ukweli,Na kudai huku si wazanzibari pekee hata Watanganyika wana haki pia ya kutaka kufahamu uhalali wa muungano. Wazanzibar msichoke kudai haki zenu kwani ni haki yenu kikatiba.
    Mpaka rais Amani Karume anastaafu hajaiona hati ya muungano ni wazi kuwa muungano huu ulikuwa wa mizengwe.
    Tunaambiwa mambo ya muungano yalikuwa kumi na moja lakini sasa yapo kama utitiri tunataka tuione hiyo hati ili kuondoa mizengwe hii.

    ReplyDelete
  4. Its time to rectify the wrong that was created by the executive in 1964. The Constitutional Petition No. 1 of 2013 shall settle this historical mistake.

    ReplyDelete