Na Stella Aron
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),
limeunda kikosi kazi maalumu (Special Task Force) kwa ajili ya uchunguzi juu ya
tuhuma za wizi wa umeme kwenye minara ya simu nchini.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
kwenye vyombo vya habari jana Dar es Salaam na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,
TANESCO imesema kuwa tayari kikosi kazi hicho kimeanza kazi kupitia minara yote
ya makampuni ya simu nchini
. Alisema uchunguzi wa awali unaonesha
kuwa kuna upotevu wa mapato ya shirika katika baadhi ya minara hiyo.Taarifa hiyo imesema kuwa kutokana na
taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari kuhusu upotevu wa umeme kwenye
minara ya simu unafuatiliwa kwa kina na kufanya ukaguzi kwenye minara yote ili
kubaini ukweli kuhusu hujuma hizo.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa uongozi wa
shirika unaahidi kuwa uchunguzi wa tuhuma hizo utakuwa huru, wa wazi na
usiomuonea mtu au kampuniyoyote . Ilisisitizwa ku wa u chunguzihuo utaf
anyikakitaalamunakwaumakini mkubwa.Ilieleza kuwa uchunguzi
utakapokamilika, kampuni za simu zitakazobainika kuiba umeme zitalazimika
kulipia kiasi chote cha umeme uliotumika bila kulipiwa pamoja na riba kwa
kipindi chote.
Sakata la hujuma kwenye minara
liliibuliwa na Majira wiki iliyopita wakati maofisa wa TANESCO walipofanya
operesheni ya kukagua minara wilayani Ilala.Wakati ukaguzi huo ukifanyika ili
kubaini hujuma baadhi ya waandishi wa habari walifika, lakini mmoja wa maofisa
wa TANESCO aliwazuia kwa madai kuwa wamepata maelekezo kuwa hawatakiwi kuwepo.
Baada ya kufanyika ukaguzi kwenye
minara miwili, walibaini kila mnara kuwa na mita mbili. Wakati huo huo, habari
za uhakika ambazo Majira imepata zimeeleza kuwa wafanyakazi wa TANESCO
walioshiriki operesheni ya kuibua wizi huo kupitia kwenye minara wametishiwa
kufukuzwa kazi.
Akizungumza na Majira kwa njia ya simu
hivi karibuni jana, Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo, alisema Wizara imeiagiza bodi na menejimenti kufuatilia na kutoa
taarifa serikalini."Tumeielekeza
bodi ifuatilie suala hilo na baadaye itatupa majibu," alisema Profesa
Muhongo
No comments:
Post a Comment