29 March 2011

Wananchi waandamana kudai 'tiba ya Mbeya'

Na Charles Mwakipesile, Mbeya

SERIKALI Mkoa wa Mbeya jana ilisalimu amri kwa mganga aliyeibuka akitibu magonjwa mbalimbali, Jafari Welino (17) na kujikuta ikibariki huduma baada ya wagonjwa
wanaotegemea huduma hiyo kuandamana na kutishia kulipua Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

Taarifa ya awali iliyolifikia gazeti hili (soma uk. 9) ilisema kuwa Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ilikuwa imemzuia kijana huyo  kutoa huduma ya tiba kwa madai kuwa mazingira ya utoaji wa huduma hiyo ni machafu na kuwa dawa anayotumia ilitakiwa ifanyiwe uchunguzi ili kuona kama ni kweli inaweza kuponya magonjwa sugu bila kuleta madhara kwa afya za binadamu.

Kutokana na hali hiyo, baada ya wagonjwa waliokuwa wamefika nyumbani kwa kijana huyo eneo la Mabatini, kilomita 2.5 kutoka katikati ya Jiji la Mbeya wakiwa na vikombe mikononi walikubalina kuandamana makubwa kwenda kwa mkuu wa Mkoa  wa Mbeya.

Kutokana na hoja za nzito za wananchi hao, na ushuhuda kuwa wengine wameponywa na kijana huyo baada ya kunywa vikombe viwili vya dawa huku wakitishia kufanya fujo kubwa ikiwa hataruhusiwa, serikali ya mkoa ilisalimu amri na kumruhusu.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. John Mwakipesile alitoa amri kwa kijana huyo kuendelea kutoa huduma huku idara zinazohusika zikifuatilia kuona namna ambayo itafanya, ili kijana huyo aweze kutoa huduma katika hali ya usafi wakati utafiti wa dawa hizo ukiendelea.

Tamko hilo liliamsha shangwe kwa wananchi hao, kisha Katibu Tawala Msaidizi Bw. Moses Chitama, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa aliongozana na waandamanaji hao kwenda nyumbani kwa kijana huyo kukagua eneo la huduma huyo, ambapo alisema kuwa ruhusa hilo ni ya muda na kuwa kijana huyo anatakiwa kuhama kwenda sehemu safi.

Bw. Chitama alisema kuwa serikali haina ugomvi na waganga wala imani za dini, na hivyo kinachotakiwa kwa kijana huyo ni kuhakikisha anafanya kazi hizo katika mazingira safi ili kutoathiri afya za wagonjwa wake.

Akijibu maswali kijana huyo aliyeonekana mwenye ujasiri alisema kuwa yeye alipewa kazi hiyo baada ya kutokewa na mizimu ambapo alikatazwa kusoma shule na kuoneshwa mti ambao aliambiwa kuwa utakuwa ukombozi kwa watu kwa kuwapa vikombe viwili kwa siku mbili bila ya malipo.

Kuhusu kuhama katika eneo hilo, alisema kuwa hawezi kufanya hivyo kwa agizo la serikali badala yake anasubiri mizimu yake iweze kumweleza jambo hilo na sehemu ya kwenda na ndipo atakapoamua kufanya hivyo.

Alisema kuwa hadi sasa amekwishatoa hudumia kwa watu wengi na miongoni mwao wapo waliopona bila ya malipo, na hivyo kufafanua kuwa hajajitokeza kwa ajili ya kumpinga Mchungaji Ambilikile Mwasapile wa Loliondo, anayedaiwa kutoa tiba ya magonjwa simu kwa kuagizwa na Mungua. Mchungaji Mwasapile wa Kanisa la KKKT, maarufu kama Babu hutoa kikombe kimoja tu cha dawa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Bw. Advocate Nyombi alisema yeye anachoangalia ni hali ya usalama wa watu wanaomiminika katika eno hilo dogo kupata huduma, huku akitaka mamlaka nyingine zifanye kazi yake ili kudhibiti uvunjifu wa amani unaoweza kutokea.

17 comments:

  1. Tunajenga taifa la washirikina,inabidi serikali iingilie kati na kutoa ufafanuzi vinginevyo tunakoenda ni kubaya kwani yaelekea wananchi hawana tena imani na sekta ya afya,nadhani sababu ya gharama kubwa na urasimu,sikubaliani wanaodai kuwa hizi ni sera za kisaikolojia za CCM na serikali yake kuwafanya watu wasahau japo kwa muda dowans na CHADEMA.

    ReplyDelete
  2. huu kweli ni ushirikina mkubwa.

    ReplyDelete
  3. Nchi ambayo viongozi wake ni washirikina, haya ndiyo matokeo. Walikuwa wakifanya sirini lakini sasa siyo siri tena tunashuhudia wakuu wa nchi (mawaziri) wakienda kupata vikombe kwa washirikina hawa kwa kisingizio cha imani ya dini. Watanzania tumekwishalogwa na nchi hii sasa ipo mikononi mwa mkuu wa giza (shetani). Maana viongozi wetu wamekwisha chukuliwa mateka, sasa tusubiri majanga ya kitaifa yatakayotokana na hasira za Mungu aliye hai kwa kulifanya taifa hili kuwa la kishirikina. Time will tell.

    ReplyDelete
  4. oh!!!! watanzania tunaangamia tumuombe mungu ili atupe kuyajua haya mambo maana inaonyesha ni yahatari sana hivi watu wanavyokwenda huko kunywa hii dawa na wakati wanasikia kabisa huo ni mzimu umemtokea alafu wao wanakwenda tu na wanajua ni kinyume na maneno ya mungu mm namshauri ambaye hajanywa hii dawa na asinywe hata kama yuko kitandani hoi aitumainie damu ya yesu inaponya magonjwa sugu ninaandika ujumbe huu nikiwa nina uzuni sana moyoni mwangu maana ninaona jinsi watu wamungu wanavyoaangamia kwa kukosamaarifa ya mungu Ee MUNGU ITAZAME NCHI YA TANZANIA ILIVYOKUMBWA NA JANGA LA MAANABI WA UONGO NAKUOMBA UIOKOE MIKONONI MWA IBILISI AMEN

    ReplyDelete
  5. hii inaonyesha watanzania wengi ni wagonjwa, kwa haraka haraka utafiti niliofanya, makanisa mengi ya uponyaji kama kwa kakobe, Mwingira, Lusekelo sasa hivi waumini wamepungua, kumbe yalikuwa yanajaa wagonjwa wenye shida mbalimbali, wakienda kwa Babu wakirudi hawrudi tena kwenye makanisa hayo wanarudi kwenye imani zao za zamani, unalifahamu hilo? pita pale mwenge kama huamini utaniambia.Tunaomba wanaopata kupona watueleze kama kweli Mbona hatuwaoni Kutangaza? sasa Mbeya nako, Moshi sijui itafuatia wapi, isiwe Musoma huko Wataua hao Jamaa hawana mchezo watafyeka huyo mponyaji.

    ReplyDelete
  6. Hao ni Wagonjwa wameandamana na serikali ya vilaza imesalimu amri je wazima wasioumwa wakiandamana kudai haki zao itakuwaje?

    ReplyDelete
  7. Mimi nadhani hawa waliojitokeza baada ya mchungaji nawaona kama washirikina na wafuasi wa shetani ambae akiona nguvu ya Mungu inatawala nae hujitokeza kuipinga au kufanya kazi sawa na hiyo ingawa hashindi,nakumbuka mfano wa Musa na Fimbo yake iliogeuka nyoka na wachawi wa misri nao wakafanya hivo hivo ingawa fimbo ya Musa iliwameza nyoka wa wachawi.najiuliza kama ni kweli kwann hawakujitokeza mda wote? Tuwe makini mizimu manake ni mashetani au ushirikina huo.

    ReplyDelete
  8. hii ni mzuri sana, bora wewe kijana umesema ukweli umeoteshwa na mizimu kuliko hao wengine wanamsingizia mungu. maana akili ya kawaida ya binadamu aliye makini kukubari kuwa mungu ndiye kakuotesha inakuwa taabu. maana sidhani kama kuna mtu ameshawahi kuongea,kumuona au kusikia sauti ya mungu kwa wakati huu tulionao. bora kijana umesema kweli ni mizimu.serikali isaidie kijana ili aweze kutoa tiba yake maana itapunguza shida na gharama wanazopata watu kutoka mikoa ya kusini kwenda mpaka loliondo kwa babu na kama yupo mwingine eneo jingine na ajitokeze ili watu wapate huduma bila ya kusafiri mbali. kwa wale wagonjwa wa magonjwa sugu waende kujaribu matibabu haya,kwani kutokwenda au kwenda hakuna cha kupoteza, ukikataa kwenda je dawa ya kupona hayo magonjwa ipo? bora ukajaribu uenda ukafanikiwa kuliko kukaa kusubiri kifo. tusiache kujaribu maana wanaofanikiwa siku zote ni wale wanaopoteza kwa kujaribu.

    ReplyDelete
  9. Damu ya YESU inanitosha. Sihitaji kikombe cha Babu wala viwili vya Kijana wa Mizimu. Kule Rombo mwingine kasema ameoteshwa na Bikira Maria! Haya...wengi watatokea...bali wale wamgojao Bwana watapata nguvu mpya, watapiga mbio wala hawatachoka, watakwenda kwa miguu wala hawatazimia! Mimi na nyumba yangu tutamngoja Bwana. Yesu ni muweza wa Yote. Alitupa Jina lake na kutoa Damu yake.

    ReplyDelete
  10. ggggmimi ngddxddttr..........
    quishney????????????
    hata mimi nitaanza kutoa baada ya babu kuchoka, mwezi wa saba......yangu itatibu magonjwa yote unayoyafahamu. kaeni mkao wa kula...usiogope kunywa kikombe sababu hata yesu alisema " kiingiacho si najisi bali kitokacho" ar u there?

    ReplyDelete
  11. na mwisho wa dunia hii ni 2012 mwezi wa 7 tarehe 29. wewe unashangaa kwanini watu wanaoteshwa kutoa dawa kwa wing? ifikapo siku ya kiama 2012 ambapo dunia itaangamizwa basi tufe wote tukiwa salama kabisa coz mbinguni hakuna kwenda ukiwa mgonjwa kabisa..... magonjwa yote yatabaki duniani kwa wale ambao yesu masihi atawakuta wakiwa hai kipindi hicho. kwa maana hiyo jitahidi ukipiga kikombe kimoja ukapona basi umenteini hadi 29/7/2012 ukiwa msafi kimwili..............

    ReplyDelete
  12. mh! nakupa pole sana wewe unayesema mwisho wa dunia ni 29/7/2012 neno la mungu linasema hukuna ajuaye siku wala saa ajapo mwana wa adamu hata malaika wenyewe walioko huko juu hawijui ila pekee mungu ndiye aanayeijua hiyo siku kwa hiyo tusijidanganye wenyewe tukisema wmisho wa dunia wakati umeshindwa kujua siku ya kufa kwako leo ukajue wmisho wa dunia kila mwanadamu inampasa amtegeme mungu peeke lkn inasikitisha watu wakiitumainia mizimu mara bikira maria nn hii? na nini mwisho wa haya ni nini?mm kitu ninajua yupo mwanaume mmoja tu aliyesimama kisha akasema yote yamekwisha naye ni YESU wengine wote wamekuja ili kujaribu imani zetu usikubali ukadanganywa

    ReplyDelete
  13. Tunamuomba mwenzi Mungu atupehekima na maarifa ili mambohaya yanayo ikabilinchi hii tuweze kupambanua mema na mabaya sijui tunakokwendaitakuwaje kama hali ndiyohii.naombaserikari ituhakikishie kama watu wanapona wanpotumia dawahizi za kuoteshwa!!!! zilizoibuka hasa mwaka huu.pia nahoji selikari kwanini isipeleke huduma yakuwapima wagonjwa katika vituo vya haowanaooteshwa ilikuutangazia umma kuwa nikweli inaponya au la.hii nihatarisan maana wengi wataoteshwa kila konaya tanzania tusipokuwamakini maana sasa bado mtume muhamed haja oteshayeyote.amakweli unabii unatimia.msukuma.

    ReplyDelete
  14. Hivi hii nayo kweli? Mungu wangu tunayo kazii ya kufanya!! na huyu kijana naye? tufuate nini? anamfuatisha babu au? anyway kama ni ya Mungu tutaona na kama ya wanadamu yatakoma tu! tuwape muda tutaona?

    ReplyDelete
  15. Shetani hana adabu hata kidogo! Karne hii kuna watu bado wanaweza kuandamana wakishinikiza kutibiwa na mganga wa kienyeji
    aliyekiri kuelekezwa tiba na mizimu yaani mapepo!Hebu fikiri kidogo mzimu ambao unazuia mtu kusoma je unakutakia mema? Viongozi watakaokwenda huko hawatufai maana wataelekezwa kulitia ujinga Taifa letu.

    ReplyDelete
  16. sijawahikuona nchi kamahii viongozi kumuunnga mkono ibilisi mtakuja kuona shetani atakavyo waaibisha.msukuma.

    ReplyDelete
  17. Watoa michango humu wote hamjaumwa nyie, ndio maana mna kejeli na kuponda, ngoja mpate ukimwi au kansa, mtakwenda hata kama ni kileleni kilimanjaro kwenye baridi kali! unafanya machezo na maradhi sugu! hata ukiambiwa sumu ya panya huponyesha utakunywa tu!

    ReplyDelete