- MAPYA YAIBULIWA
Na Mwandishi Wetu
SAKATA la jengo la Golden Plaza lililopo
Mtaa wa Agrey na Indira Gandh jijini Dar es Salaam limezidi kuchukua sura mpya
kutokana na wapangaji wa jengo hilo kuonesha kasoro kubwa zilizopo kwenye jengo
mbali na nyufa zinazoashiria kwamba linaweza kuanguka wakati wowote.Akizungumza na
gazeti hili mmoja wa wapangaji katika jengo hilo (jina tunalo) alisema jengo
hilo limejengwa na taasisi mbili (majina tunayo).
Alisema jengo
hilo lina wapangaji wanaolitumia kama ofisi na makazi ya watu zaidi ya 70.
Alisema ghorofa mbili ndizo zinazotumika kwa ajili ya maduka na ofisi.Alisema yeye
ndiye mpangaji wa kwanza katika jengo hilo na amekuwa akipeleka malalamikahusika bila hatua kuchukuliwa.
"Tumelalamika
matatizo ya jengo hili lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa,"
alisema.
Mpangaji
mwingine (jina tunalo) alisema jengo hilo lina matatizo mengi yakiwemo ya
baadhi ya vifaa vilivyotumika kulijenga kuangua chini.Majira ilishuhudia baadhi ya vyumba vya
wapangaji vikiwa na miinuko ambapo marumaru zilizowekwa chini badala ya sakafu
zimebanduka na kusababisha miinuko.
Mbali na hilo pia katika ghorofa ya
pili ya jengo hilo imejaa maji kutoka kwenye mabomba yanayotoka ghorofa ya juu
na kusababisha maji kutuama.Mmoja wa wapangaji alisema hali ni
mbaya katika baadhi ya ghorofa za jengo hilo kutokana na kuwa na nyufa za
kutisha. "Kuja kufika kwenye ghorofa hizo labda mje na polisi ndipo
mjionee hali ilivyo ndani," alisema mpangaji huyo kwa sharti la jina lake
kutochapishwa gazetini.
Baadhi ya wananchi waliokuwepo karibu
na jengo hilo, walisema kwa sasa lazima mamlaka husika zifanye kazi kwani
inaonekana jengo hilo halikujengwa kitaalamu.Walisema ukiliangalia jengo hilo utaona
nyufa nyingi kwani kuna marumaru zimebanduka ukutani na kuanguka na hata rangi
za ukutani zinamechakaa zina maji yanayopenya kutoka ghorofa za juu.
"Ni vyema Serikali ikawafuatilia
wahusika na kulifanyia ukaguzi wa kina jengo hili kabla halijaleta madhara
kwani wataalamu hawafiki kwa ajili ya ukaguzi na hata kama wakija hakuna majibu
wala taarifa wanazotoa kwa watumiaji wa jengo hilo," alisema mmoja wa
wananchi wenye biashara eneo hilo.
Licha ya majira kufanya jitihada kwa siku tatu
ili kupata ufafanuzi wa jengo hilo kutoka Manispaa ya Ilala na Bodi ya Usajili
wa Waandisi (ERB) lakini wahusika wa sehemu hizo wamekuwa kimya
Jengo lingine tena la NHC yenye utata.
ReplyDeletemmh jamani my Engeneer mko wpi?mmesomea nini vyuoni?mbona mnataka kuuwa wananchi wetu kwa ajili ya tamma zenu za hela, mungu awasamehe kwa ababu hamui mlitendalo
ReplyDeleteHatari sana.serikali lazima ichukue hatua kali
ReplyDelete