30 July 2013

WAKILI AKWAMISHA KESI YA KIBANDA



Na Rachel Balama
KE S I i n a y o m k a b i l i aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda jana imeshindwa kuendelea kutokana na wakili wa upande wa Jamhuri anayeshughulikia kesi hiyo kutofika mahakamani hapo. Jana ilikuwa tarehe ya mwisho kwa upande wa Jamhuri kuieleza mahakama kama wanaendelea na ushahidi au wanafunga baada ya mahakama kutoa agizo hilo Julai 15, mwaka huu.

Wakili wa Serikali, Beatha Kitau, aliiomba mahakama iahirishe kesi hiyo kwa kuwa wakili wa Serikali Tumaini Kweka anayesimamia kesi hiyo kutofika mahakamani hapo.
Baada ya ombi hilo Hakimu Mkazi Waliarwande Lema aliahirisha shauri hilo hadi Agosti 14, mwaka huu.
Mbali ya Kibanda ambaye kwa sasa ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari 2006, washtakiwa wengine ni aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa gazeti la Mwananchi, Theophil Makunga na mwandishi wa makala, Simon Mwigamba.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kuruhusu na kuchapisha makala ya uchochezi katika gazeti la Tanzania Daima iliyokuwa na kichwa cha habari "Waraka maalum kwa askari wote".

No comments:

Post a Comment