Frank Monyo na Theophan Ng'itu
JESHI la Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 38 kwa makosa mbalimbali
yakiwemo kukutwa na nyara za Serikali, wizi wa magari pamoja na funguo bandia. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamishna wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema Julai 22, mwaka huu maeneo ya
Msimbazi Center polisi wakiwa doria walimtia mbaroni mkazi wa Mwananyamala,
Ibrahimu Mnyanga akiwa na meno ya tembo vipande 16 vyenye kilo 24.5.
Pia alisema, walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine watatu
wakiwa na vifaa vya milipuko kwenye nyumba ya Rose Amel, mkazi wa Salasala
wilayani Kinondoni. Kova alisema kuwa, watuhumiwa wengine sita walikamatwa na magari
matatu yenye namba za usajili T 723 BXF aina ya Verossa likiwemo T 220 BPE aina
ya Toyota Pasoo na T 823 CCS aina ya Suzuki maeneo ya Keko Magurumbasi Wilaya
ya Temeke na Kikosi cha Kudhibiti Wizi wa Magari.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Omari Kaisi, mkazi wa Keko,
Mohamed Seif, mkazi wa Yombo Kilakala, Abubakari Rashidi, mkazi wa Kiwalani
Minazi Mirefu, Shabani Ngonde, mkazi wa Kinondoni Mkwajuni na Shabani Rajabu
mkazi wa Tabata.
Kamanda Kova alisema kuwa, polisi wamejipanga kuimarisha ulinzi
katika msimu huu wa sikukuu ya Idi inayotarajiwa kufanyika Agosti 8, mwaka huu.
Alisema, Jeshi la Polisi limejipanga kikamilifu kuhakikisha ulinzi
unakuwepo maeneo yote ya fukwe za bahari, kumbi za starehe na kuhakikisha
linadhibiti vitendo vyote vya uhalifu
No comments:
Post a Comment