25 July 2013

TAMWA KUZINDUA RIPOTI YA UNYANYASAJI



 Na Rehema Maigala
CHAMA cha Wanahabari Wa n a w a k e Ta n z a n i a (TAMWA) leo kitazindua ripoti ya utafiti wa unyanyasaji wa kijinsia uliofanyika Aprili mwaka huu katika wilaya 10 za Tanzania Bara na Zanzibar.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari jana Dar es Salaam imesema kuwa ripoti hiyo ni utafiti unaoonesha hali halisi ya unyanyasaji wa kijinsia katika jamii pamoja na mambo yanayokwamisha juhudi za vyombo vinavyotetea haki za wanawake na watoto hapa nchini

Taarifa hiyo imesema kuwa utafiti huo ulifanywa kwa kushirikiana na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya Nipashe, The Guardian, The Citizen, Mwananchi, Daily News, Zanzibar Leo na Majira.Ilisema kuwa waandishi wa habari waliweza kuwahoji wanajamii mbalimbali kuanzia ngazi za familia na kupata ukweli wa hali halisi ya unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo, ukeketaji, ubakaji, wanawake na watoto kutelekezwa, mimba katika umri mdogo na watoto wa kike
 kulazimishwa kuolewa.
I l i e l e z a k u w a w i l a y a ziliyofanyiwa utafiti ni pamoja na Wete (Pemba Kaskazini), Unguja Mjini Magharibi (Unguja Magharibi), Unguja Kusini, Kisarawe (Pwani), Newala (Mtwara), Mvomero (Morogoro), Lindi vijijini na Ruangwa (Mtwara), Kinondoni na Ilala Dar es Salaam.Uzinduzi wa ripoti hiyo ya utafiti ni mwendelezo wa utekelezaji wa mradi wa kujenga na kuimarisha usawa wa kijinsia na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (GEWE II) unaoshirikisha mashirika yanayotetea haki za jamii hasa wanawake na watoto yakiwemo TAMWA, Jumuiya ya Wanawake Wanasheria Zanzibar ZAFELA, Chama cha Wanasheria Wanawake ñ TAWLA, Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), na Kituo cha Usuluhishi cha TAMWA (CRC).

No comments:

Post a Comment